HabariHabari Tofauti

Kusherehekea maadhimisho ya miaka 119 ya kuanzishwa kwa Makumbusho ya Jumba La Manial

Ali Mahmoud 

Makumbusho ya Jumba la mwana-mfalme Mohammed Ali katika El Manial kwa kushirikiana na usimamizi mkuu wa vituo vya akiolojia kwenye Baraza kuu la Vitu vya Kale, yanaandaa maonesho ya akiolojia kwa mwezi mmoja kusherehekea maadhimisho ya miaka 119 ya ujenzi wa Jumba hilo.

Mo’men Othman, mkuu wa sekta ya makumbusho katika Baraza Kuu la Vitu vya kale, alisema kuwa maonesho yanajumuisha karibu vitu 70 vya kale vya aina mbalimbali vilivyodhibitiwa na usimamizi mkuu katika vituo hivi na sehemu za kiakiolojia kwenye bandari za Misri, la maarufu zaidi ni mtungi wa Fedha kwa binti-mfalme Tawhida binti wa Khedive Ismail, uliopambwa kwa mapambo ya mimea na kijiometri, na meza juu yake kuna mandhari yenye picha ya okestra inayozungukwa na fremu ya chuma ya dhahabu iliyopambwa na mapambo ya mimea yaliyovutia na kuenea kwa miguu, sanamu ya nusu ya Mfalme Fuad wa kwanza kutoka marumaru nyeupe, na mlazi wa Mfalme Farouk uliotengenezwa na mbao yenye dhahabu na imepambwa na mapambo ya kijiometri na mimea, na kwa pande zake ina monogram ya Mfalme Farouk na juu yake taji ya kifalme.

Kwa upande wake, Amal Siddiq, mkurugenzi mkuu wa makumbusho, aliongeza kuwa kando ya maonyesho, itapangwa muhadhara Juu ya Mwana-Mfalme Mohammed Ali na majumba ya makumbusho ambayo yatolewa na Mheshimiwa profesa Mohammed Al-Bardini, mkurugenzi wa makumbusho, pamoja na kuandaa idadi ya ziara za kuongoza na warsha za elimu na zinazohusika na watu wa uwezo maalum ya kuwajulisha kwa makumbusho na vitu vyake.

Inatajwa kwamba ujenzi wa jumba la makazi ulianza, ambalo ni jumba la kwanza kujengwa katika ikulu, kisha imeendelea kujenga majumba mengine na sehemu za ikulu, ili zijumuishe jumba la Mapokezi, mnara wa saa, Sabil, msikiti, Makumbusho ya uwindaji, jumba la makazi, jumba la ufalme, makumbusho ya pekee, jumba la dhahabu, pamoja na bustani ya ajabu inayozunguka kasri, inayosifiwa kwa mimea mingi na miti ya pekee. Kazi ya ujenzi iliendelea hadi mwaka wa 1943.

Jumba la Mwana-Mfalme Mohammed Ali Huko Manial pia ni ya kipekee katika muundo wake mzuri wa usanifu, ambapo yalijengwa kwa mitindo kadhaa ya kiislamu, kwa hivyo yanazingatiwa shule kamili ya kiufundi kwa mambo ya Sanaa na usanifu wa kiislamu, pia yako katika sehemu nzuri kwenye tawi la mashariki la Nile kwenye kisiwa cha Manial Al-Rawdah.

Yanasifiwa kwa mapambo yake mbalimbali na tofauti kutoka enzi mbalimbali za kihistoria, ambapo yana karibu mapaa 38 yenye mapambo mbalimbali, rangi na malighafi, mbali na vyombo nadra vya sanaa na vitu thamani vya kale.

Mwana-Mfalme Mohammad Ali ni mtoto wa Khedive Tawfik, na ndugu ya Khedive Abbas Hilmi wa pili, alikuwa mrithi wa kiti cha ufalme baada ya ndugu yake na alikuwa mlinzi wa ufalme baada ya kifo cha mjomba wake Mfalme Fuad wa kwanza mnamo mwaka wa 1936, na pia aliteuliwa Kuwa Mrithi wa Mfalme Farouk hadi mwaka wa 1951. Alikuwa mwenye utamaduni mkubwa, na alikuwa maarufu kwa upendo wake kwa Sanaa za kiislamu na shauku yake kwa kukusanya vitu vya kale, na alikuwa mpenda sanaa kwa aina zake zote, haswa vile vya kiislamu, na moja ya mafurahisho yake maarufu ni ufugaji wa farasi za arabia zenye asili za kale za kiarabu, na yeye alipendekeza kwamba ikulu kugeuzwa baada ya kifo chake kukawa makumbusho yanayobeba jina lake.

زر الذهاب إلى الأعلى