Habari

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AKUTANA, AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA                                       

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,  Bi Mary Maganga leo tarehe 09 Agosti,2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Kenya ,Dr. John Simbachawene ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP).

Katibu Mkuu yuko  mjini  Nairobi, kwa  ajili ya kukutana na uongozi wa UNEP ili kuwasilisha na kujadili vipaumbele vya Serikali ya Awamu sita katika Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Maeneo yatakayojadliwa katika mkutano huo ni pamoja na  jitihada za kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi, Hifadhi ya biounuai na Udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira, kama yalivyoainishwa kwenye Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wa mwaka 2022-2032.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana na UNEP katika Utekelezaji miradi, Kukuza uwezo wa Kitaasisi na Utekelezaji wa Sera  ya Mazingira.MWISHO.

زر الذهاب إلى الأعلى