Habari

Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje,Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika na Mikutano ya Kiafrika, ampokea Balozi wa Majukumu maalum katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi na Balozi wa Urusi jijini Kairo

Mervet Sakr

0:00

Balozi Ashraf Sweilem, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika na Jumuiya za Kiafrika, akimpokea Oleg Ozerov, Balozi wa Majukumu Maalum ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, na “Georgi Borisenko,” Balozi wa Urusi huko Kairo, na Mwakilishi wa Urusi katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu,ambapo Mkutano huo ulijadili maandalizi ya Mkutano ujao wa Wakuu wa Urusi na Afrika, utakaofanyika St. Petersburg Julai 2023.

Oleg alionesha matarajio yake ya ushiriki wa Rais Abdel Fattah El-Sisi katika Mkutano wa kilele wa Kiurusi na Kiafrika(Afro-Urusi), ikizingatiwa kuwa Misri ndio lango la kuingia Afrika na kuwa nchi kubwa na waanzilishi katika bara hilo, akisifu mafanikio ya toleo la kwanza la Mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika, ambao ulifanyika katika jiji la Urusi la Sochi mnamo 2019, na jukumu muhimu na la ufanisi lililofanywa na Misri katika kuzindua toleo la kwanza la mkutano huo, pamoja na uenyekiti mwenza wa Rais Abdel Fattah El-Sisi na Rais Putin.

Kwa upande wake Balozi Ashraf Swailem alieleza kuwa kikao hicho kilishuhudia kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya bara hilo,alitaja masuala mengi ya kimataifa kuhusiana na mustakabali wa kazi za kimataifa na mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na upanuzi wa kundi la 20 ili kuongeza uwakilishi wa Afrika, mbali na kujadili vipaumbele vya maendeleo ya bara la Afrika na kusisitiza umuhimu wa kutumia vyema matokeo ya mkutano wa kilele wa Afrika na Urusi kwa njia inayoonesha manufaa kwa pande zote mbili na kufikia maslahi ya pamoja.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"