Habari

Rais El-Sisi ampokea Rais Al-Ghazwani

Mervet Sakr

Rais Abdel Fattah El-Sisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kairo, alimpokea Rais Mohamed Ould Ghazouani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, mwanzoni mwa ziara yake ya siku tatu nchini Misri, kisha akaongozana na Rais wa Mauritania kwenye Kasri la Ittihadiya, ambapo sherehe rasmi ya mapokezi ilifanyika, walinzi wa heshima walipitiwa na nyimbo za taifa zilichezwa.

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Misri, Mshauri Ahmed Fahmy, alisema kuwa Marais hao wawili walifanya mazungumzo ya kibinafsi, na kufuatiwa na kikao kilichopanuliwa cha mazungumzo kilichojumuisha wajumbe wa nchi hizo mbili, ambapo marais hao wawili walithamini maendeleo endelevu katika mahusiano ya Misri na Mauritania na maendeleo thabiti yaliyoshuhudiwa na mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili ndugu mnamo miaka ya hivi karibuni katika ngazi zote, haswa kuhusiana na jeshi, usalama na kupambana na ugaidi katika kanda ya Sahel.

Marais hao wawili pia walijadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kubadilishana biashara na kuongeza uwekezaji baina ya nchi hizo mbili mnamo kipindi kijacho, ambapo Rais wa Mauritania l katika suala hilo alisifu uzoefu wa maendeleo ya Misri, akielezea shukrani kwa msaada wa Misri na kujenga uwezo na makada kwa ndugu wa Mauritania katika nyanja zote.

Katika muktadha huu, ilikubaliwa kuitisha Kamati ya Pamoja ya Juu katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje Julai ijayo, wakati ambapo mikataba kadhaa ya ushirikiano itasainiwa katika nyanja mbalimbali, kwa njia inayoongeza mifumo ya ushirikiano wa Misri na Mauritania na ushirikiano na kufikia maslahi ya watu wawili.

Msemaji huyo aliongeza kuwa mkutano huo ulishuhudia kubadilishana mawazo juu ya utaratibu wa kuendeleza hatua za pamoja za Kiarabu na Afrika, wakati wa kujadili maendeleo katika masuala kadhaa ya kikanda, haswa Sudan, Libya, Syria na Bwawa la Al-Nahda.

زر الذهاب إلى الأعلى