Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Waziri mwenzake wa Comoro pembezoni mwa kazi za Baraza Kuu la Umoja wa Afrika
Ali Mahmoud
Bw. Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, alikutana Jumatano, Februari 15, 2023, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, “Dahir Zul-Kamal”, pembezoni mwa kushiriki katika kazi ya kikao cha 42 cha Baraza Kuu la Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa.
Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alimpongeza mwenzake kwani nchi ya Comoro ilichukua urais wa Mzunguko wa Umoja wa Afrika kwa mwaka mmoja, na hivyo wakati wa Mkutano wa Kilele wa Umoja huo uliopangwa kufanyika mnamo siku za 18-19 Februari hii, akielezea imani ya Misri katika uongozi wa Comoro kwa Umoja wa Afrika katika hatua hiyo wakati Bara linakabiliwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi na usalama. Waziri Shoukry pia alisisitiza msaada wa Misri kwa Urais wa Comoro kwa Umoja huo, na matarajio ya uratibu na kazi ya pamoja kuelekea kuimarisha kazi ya Pamoja ya Afrika chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika.
Balozi Abu Zeid aliongeza kuwa mkutano huo pia ulishughulikia kujadili masuala mengi ya mahusiano ya pande mbili kati ya Misri na Comoro, na kujenga juu ya mkutano wa viongozi wa nchi hizo mbili nchini Misri mnamo mwaka wa 2019 wakati wa uongozi wa Rais wa Comoro kwa ujumbe wa nchi yake katika Jukwaa la Aswan la Maendeleo na Amani Endelevu.
Waziri wa Mambo ya Nje ametoa mwaliko kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro kutembelea Misri ili kuendeleza ushirikiano wa pamoja. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alielezea kuwa Bw. Sameh Shoukry alisisitiza nia ya Misri kwa kuimarisha ushirikiano na Comoro katika nyanja za kiuchumi, biashara, uwekezaji na kiufundi, na kutarajia kuimarisha jukumu la kampuni za Misri katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya “mpango wa Comoro unaojitokeza 2030”, pamoja na ushirikiano katika nyanja za uvuvi wa baharini na uanzishaji wa mashamba ya samaki, na utoaji wa Misri kwa msaada katika uwanja wa kujenga uwezo na uhamisho wa maarifa kupitia programu nyingi za mafunzo zilizoandaliwa na Shirika la Misri la Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo, pamoja na misaada iliyotolewa na Al-Azhar Al-Shareif na Wizara ya Elimu ya Juu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alihitimisha taarifa zake, akiashiria kuwa mawaziri hao wawili walikubaliana mwishoni mwa mkutano kuimarisha mashauriano na uratibu mnamo kipindi kijacho katika mfumo wa utashi wa pamoja wa kuimarisha kazi chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika.