Waziri wa Mambo ya Nje ajadiliana na Mwenzake wa Chad masuala yenye maslahi ya pamoja pembezoni mwa kazi za Baraza la kiutendaji la Umoja wa Afrika
Ali Mahmoud
Waziri wa Mambo ya Nje, Sameh Shoukry, siku ya Jumatano, Februari 15, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad “Mohamed Salih Al-Nadif” pembezoni mwa kikao cha 42 cha Baraza la kiutendaji la Umoja wa Afrika.
Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa mawaziri hao wawili walijadiliana njia za kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili katika nyanja mbalimbali, pia Waziri Shoukry alisisitiza msaada wa Misri kwa mchakato wa mazungumzo ili kufikia utulivu huko N’Djamena, akisisitiza utayari wa Misri kutoa aina zote za msaada katika hatua hiyo, ikiamini jukumu muhimu la Chad katika eneo. Waziri Shoukry pia alimfahamisha mwenzake juu ya maoni ya Misri kuhusu masuala kadhaa na mada zilizowasilishwa kwenye ajenda ya Baraza la Utendaji na Mkutano wa Kilele wa Afrika, na wamebadilishana maoni juu ya masuala kadhaa na migogoro ya kisiasa na ya usalama katika ngazi ya Bara.
Msemaji rasmi huyo alifafanua kuwa mawaziri hao wawili walijadili njia za kuamsha jukumu la jumuiya ya sahel na jangwa, haswa kwa kuzingatia machafuko na changamoto za usalama zinazokabili kanda hiyo, na walikubaliana kuendelea mashauriano na uratibu katika suala hilo.