Chuo kikuu cha Kairo chatangaza kushinda kwa wanasayansi 41 kwa Tuzo za Chuo Kikuu Mwaka 2022
Ali Mahmoud
Dkt. Elkhosht: tume za upatanishi zilijumuisha maprofesa wakuu kutoka kwa Vyuo Vikuu vya Misri
Chuo kikuu cha Kairo, kikiongozwa na Dkt. Mohamed Othman Elkhosht, Mkuu wa Chuo Kikuu, kimeidhinisha majina ya washindi wa tuzo za Chuo kikuu kwa Mwaka 2022, kwa aina zake: Ubora wa kisayansi, Shukrani, Ufanisi wa kisayansi, kutia moyo, uvumbuzi, tuzo ya Naguib Mahfouz kwa ubunifu wa kiakili na fasihi, na tuzo ya binti-mfalme Fatima, ambapo wanasayansi na watafiti 41 kutoka sekta mbalimbali za kitaaluma walishinda tuzo hizo.
Dkt. Mohamed Elkhosht alisema kuwa tume za upatanishi zilijumuisha maprofesa wakuu kutoka Vyuo Vikuu vya Misri, akiashiria kuwa vigezo vya tuzo za Chuo Kikuu vimeboreshwa viendelee sambamba na mabadiliko ya kimataifa katika utafiti wa kisayansi, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa idadi ya vigezo vipya kama vile usasa na ubora kuhusu utafiti wa kisayansi, na uhusiano wa utafiti wa kisayansi na mipango ya maendeleo endelevu, kama Chuo kikuu miongoni mwa Vyuo Vikuu vya kizazi cha nne.
Katika tuzo za ubora, ambazo ni tuzo moja kwa kila uwanja kutoka nyanja saba, Dkt. Mona Fouad Ali Abdel Ghani kwenye Kitivo cha Akiolojia alishinda katika uwanja wa sayansi za kibinadamu na kielimu, Dkt. Hassan Abdel Basset Mohamed kwenye Kitivo cha Sheria katika uwanja wa Sayansi za Jamii, Dkt. Yousef Fawzi Rashid kwenye Kitivo cha Uhandisi katika uwanja wa Sayansi za Uhandisi, Dkt. Olfat gamil shaker kwenye Kitivo cha Tiba katika uwanja wa sayansi za tiba na maduka ya dawa na Dkt. Gamal sayed Ali Al-barouti kwenye Kitivo cha Kilimo katika uwanja wa sayansi za taaluma mbalimbali, Dkt. Fakiha Mohamed El-Tayeb kwenye Kitivo cha Sayansi katika uwanja wa sayansi za juu za teknolojia, na tuzo katika uwanja wa sayansi za msingi ilizuiliwa kulingana na makadirio na maksi za tume za wasuluhishi.
Katika Tuzo za Chuo Kikuu za Shukrani na idadi yake ni tuzo moja kwa kila uwanja kutoka nyanja saba, Dkt. Alaa Eldin Abdul Moaty Mohamed, Kitivo cha Tiba ya wanyama, sawa na Dkt. Salama Abu Al-Yazid Auf, Kitivo cha Sayansi katika uwanja wa sayansi za taaluma mbalimbali, Dkt. Al-Hussein Mohamed Abdul-Moneim Al-Sayed kwenye Kitivo cha Sanaa katika uwanja wa sayansi za kibinadamu na za kielimu, Dkt. Mohamed Mahmoud Mohamed Youssef kwenye Kitivo cha Biashara katika uwanja wa sayansi za jamii, Dkt . Muhy Saad Abdul-Hamid Mansour, Kitivo cha Uhandisi katika uwanja wa sayansi za uhandisi, Dkt. Fouad Abdul-Moneim Abdullah, Kitivo cha Tiba katika uwanja wa sayansi za tiba na maduka ya dawa Dkt. Nada Farouk Ahmed Atta, Kitivo cha Sayansi katika uwanja wa sayansi za juu za teknolojia na tuzo ilizuiwa katika uwanja wa sayansi za msingi kulingana na alama na makadirio ya tume za wasuluhishi.
Na kuhusu tuzo za Chuo Kikuu kwa ubora wa kisayansi, ambazo idadi yake ni tuzo moja kwa kila uwanja kutoka nyanja nane, Dkt. Safa Abdulkader Mohamed Hamed, Kitivo cha Akiolojia, alishinda tuzo katika uwanja wa Sayansi za kibinadamu na kielimu, Dkt. Marwa Mohamed Shebl, Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa, katika uwanja wa Sayansi za Jamii, Dkt. Mahmoud Mohamed Kamel, kwenye Taasisi ya Kitaifa ya Vivimbe katika uwanja wa sayansi za tiba na maduka ya dawa, na Dkt. Ehab Reda Ahmed Mohamed kwenye Kitivo cha Kilimo, katika uwanja wa sayansi za kilimo, na tuzo hiyo ilizuiliwa katika nyanja za: sayansi za msingi, sayansi za uhandisi, sayansi za taaluma mbalimbali, na sayansi za juu za teknolojia.. Kulingana na alama na makadirio ya wasuluhishi.
Tuzo za Chuo Kikuu za kutia moyo na idadi yake 26 katika nyanja 10, Dkt. Sayed Rashad Qorany Mohamed kwenye Kitivo cha Masomo ya Kiafrika alishinda katika uwanja wa sayansi za kibinadamu na kielimu, na Dkt. Siham Kamal Mohamed Abdel Aal, kwenye Kitivo cha Sayansi katika uwanja wa sayansi za fizikia. Na katika uwanja wa sayansi za kemikali, Dkt. Sally Al-Sayed Ahmed Ashouri Al-Ashry, kwenye Kitivo cha Sayansi, na Dkt. Yousef Mohammed Ahmed kwenye Kitivo cha Sayansi walishinda, na katika uwanja wa sayansi za kemikali, kati ya Dkt. Huda Kamel Mahmoud Sayed na Dkt. Marwa Al-Badri Mohamed Khalifa kwenye Kitivo cha sayansi. Na katika uwanja wa sayansi za biolojia, alishinda kwake Dkt. Amr Adel Abdul Khaliq, kwenye Kitivo cha Sayansi na Dkt. Ola Sayed Ahmed kwenye Taasisi ya kitaifa ya Vivembe. Na katika uwanja wa sayansi za kilimo, alishinda kwake Dkt. Essam Mohamed Abdul Aleem Abdul Salam kwenye Taasisi ya kitaifa ya Sayansi za Liza, na Dkt. Marwa Ibrahim Abdul Hamid, kwenye Kitivo cha Tiba ya wanyama, Dkt. Marwa Mohamed Attiya, kwenye Kitivo cha Tiba ya wanyama, Na Dkt. Mahdi Sayed Mahdi Al-Sayed kwenye Kitivo cha Kilimo. Na katika uwanja wa Sayansi za kitiba, walioshinda ni Dkt. Asmaa Al-Sayed Abdul Latif kwenye Kitivo cha Dawa, Dkt. Marwa Adly Mohamed Saleh kwenye Kitivo cha Tiba, Dkt. Zainab Abdul Latif Mahmoud kwenye Kitivo cha Tiba, Na Dkt. Iman Desouki Taha kwenye Taasisi ya Kitaifa ya Vivembe. Na katika uwanja wa sayansi za uhandisi, walioshinda ni Dkt. Mohamed Mohy Mohamed Saad, katika Kitivo cha Uhandisi, Dkt. Omnia Hamdi Abdul Rahman, kwenye Taasisi ya Kitaifa ya Sayansi za Liza, Dkt. Safwat Mahmoud Safwat, kwenye Kitivo cha uhandisi, Na Dkt. Hebatullah Essam Eldin, kwenye Kitivo cha Uhandisi. Na Tuzo hiyo ilizuiliwa katika nyanja za Sayansi za Jamii na sayansi za kijiolojia kulingana na alama na makadirio ya wasuluhishi.
Na aliyeshinda Tuzo ya Naguib Mahfouz kwa ubunifu wa kiakili na fasihi, Dkt. Mai Yousef Abdul Qader Khalif katika Kitivo cha Sanaa, na alishinda kwa Tuzo ya binti-mfalme Fatima, Dkt. Nawal Abdul Raouf Mustafa kwenye Kitivo cha tiba za kiasili.
Na kuhusu Tuzo ya Chuo Kikuu kwa uvumbuzi, ambayo hutolewa kwa kila mtu ambaye amepata haki ya ubuni na masharti yanamtumika, alishinda kwake Dkt. Dalia Jalal Mustafa Saeed katika Kitivo cha Uhandisi, sawa na Dkt. Hossam Mohamed Abdul Hamid kwenye Kitivo cha Uhandisi.