Uwanja wa Alexandria
Ni uwanja mwenye matumizi mbali mbali, amabao uko mjini Alexandria katika Mtaa wa Muharam Bik nchini Misri, lakini hivi sasa unatumiwa katika mechi za mpira wa miguu.
Uwanja huu ni uwanja rasmi wa Timu ya Al-Itihad, Timu ya Al-Olimb i na Timu ya Sumuha.
Uwanja wa Alexandria ni uwanja wa zamani sana nchini Misri na katika Afrika, licha ya kuwa ni uwanja wa kwanza katika Ulemwengu wa Kiarabu kutumia taa.
Uwanja huo ulijengwa mwaka 1929, ambapo ulikuw na upana wa kukaliwa na mashabiki 13660, lakini baada ya marekebisho ukawa na uwezo wa kukaliwa na mashabiki 20000. Uwanja huo umefunguliwa mnamo 17 Novemba 1929, wakati huu uliitwa Uwanja wa Fuaad Al-Awal. Mfalme Fuaad Al-awal amehudhuria ufunguzi wake kupitia mechi iliyofanyika kati ya Timu ya Al-Itihad na Timu ya Cairo.
Baada ya Mapinduzi ya Julai 1952, limebadilika jina la uwanja na likawa Uwanja wa Al-Baladia, kisha limebadilika na likawa Uwanja wa Alexandria (jina la hivi sasa ).
Ulipoanzishwa ramani yake ilikuwa kwa Msanifu ujenzi wa kirusi Nikosov ambaye amechora ramani ya uwanja, ramani yenye kufanana na nembo za ushindi za kigiriki kwa mfumo zamani wa kirumi, lakini kwa njia ya kisasa.
Vile vile alichunga kuwa ramani ya uwanja kukusanya baadhi ya sehemu za kuta za mji wa zamani wa kiislamu Alexandria.
Uwanja huo umesharekebishwa mwaka 1996 kabla ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Vijana, ambapo zimefanyika huko baadhi ya mechi za michuano hiyo.
Pia umerekebishwa kabla ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Kiafrika mwaka 2006, ambayo timu ya Misri ilikuwa bingwa wa kombe hilo.
Vile vile umesharekebishwa kabla ya ufunguzi wa Michuano ya Klabu Bingwa za Kiarabu, michuano iliyofanyika nchini Misri kwenye miji miwili nayo ni ; Alexandria na kairo.