Habari

Burkina Faso yatoa nishani ya heshima kwa Balozi wa Misri

0:00

Ndani ya muktadha wa mahusiano ya nchi mbili kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Burkina Faso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Olivia Rwamba, alimzawadia Balozi Ibrahim Abdel Azim El-Khouly “Nishani ya heshima ya kitaifa na cheo cha afisa”, mapambo ya juu zaidi nchini Burkina Faso, akitambua juhudi zake za kipekee kwa miaka mitatu, na nia yake ya kuendeleza mahusiano kati ya nchi hizo mbili, iliyofikia kiwango cha juu cha ubora.

Hayo yamejiri wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Waziri wa Burkina Faso wakati wa kumalizika kwa ujumbe wa “El-Khouly” kama balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa serikali ya Burkina Faso, na sherehe hiyo ilihudhuriwa na kundi la maafisa waandamizi wa serikali, Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso na mabalozi kadhaa wa Kiarabu na wa kigeni.

Wakati wa hotuba yake, Waziri wa Burkina alisifu juhudi za Balozi wa Misri mnamo kipindi kizima cha miaka mitatu ya kushika madaraka yake, na kujitolea kwake katika kukuza mahusiano ya Misri na Burkini, yaliyoshuhudia kushamiri hivi karibuni, Pamoja na mashauriano na uratibu endelevu kati ya pande hizo mbili, na kubadilishana usaidizi katika faili zote na uteuzi. Pia alisifu msimamo wa Misri pamoja na Burkina Faso katika vita vyake dhidi ya ugaidi na kuisaidia kushinda changamoto za sasa. ‏

Kwa upande wake, Balozi huyo wa Misri alielezea fahari yake kwa miaka aliyotumia kutumikia maslahi ya nchi hizo mbili, na akasifu ushirikiano na uratibu unaoendelea kati ya nchi hizo mbili za kidugu, akibainisha shukrani zake kubwa kwa Burkina Faso kama rais, serikali na watu na matakwa yake ya utulivu, ustawi na maendeleo.

Ikumbukwe kuwa Rais Ibrahim Traoré, Rais wa mpito wa Burkina Faso, alikuwa amepokea siku chache zilizopita Balozi wa Misri kumuaga na kumshukuru kwa juhudi zake wakati wa muda wake, ikifuatiwa na mikutano kama hiyo ya kumuaga balozi kutoka kwa idadi kubwa ya maafisa wa Burkina, haswa Waziri Mkuu wa Burkinabe, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sheria na Waziri wa Ulinzi.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"