Vijana Na Michezo

“Wizara ya Michezo” yaendelea shughuli za Riwaq Al-Azhar kwa watoto na familia katika vituo vya vijana

Ali Mahmoud

0:00

Wizara ya Vijana (Idara kuu maendeleo ya Wachipukizi) kupitia usimamizi mkuu wa utunzaji wa watu wenye vipawa na wabunifu, iliendelea na shughuli za Riwaq Al-Azhar kwa ajili ya watoto na familia kwenye vituo vya vijana, kwa kushirikiana na Al-Azhar Al-Shareif, pamoja na Ufadhili wa ufadhili wa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo.

Bi. Jehan Hanafi, Naibu wa Wizara, Mkuu wa Idara kuu ya Maendeleo ya Vijana, alisisitiza kuwa mpango huo unalenga kurekebisha dhana potofu za kidini, pamoja na kukuza tabia na maadili ya wachanga, vijana na familia, na kujibu maswali yanayokuja akilini mwa wachanga, vijana na familia za Misri.

Mikutano ya Riwaq katika mikoa yote ilishughulikia maadili ya Qur’ani Tukufu na jinsi ya kuyatumia.

Pia, hapo awali yamejadili maadili ya adabu ya kuomba ruhusa, adili la usafi, utii wa wazazi, kuheshimu wakati, kuheshimu mwalimu, thamani na umuhimu wa sala na kwamba ni msingi wa dini, na maadili mengine yanayopanda cheo cha maadili, na kuunganisha familia, vijana na wachanga na jinsi ya kuyatumia kwa ukweli.

Shughuli za Riwaq zilifanyika katika mikoa mbalimbali kwa ukaaji wa kweli wa wahubiri wa Al-Azhar na wachanga na vijana, ndani ya vituo vya vijana kwa lengo la kuona tabia na kufanya kazi kwa ajili ya kuirekebisha, haswa kwa sababu vituo vya vijana katika mikoa yote kwa wakati huu vikawa vituo muhimu vya huduma za jamii, na vijana katika mikoa yote walionesha furaha zao kubwa na kunufaika kutokana na shughuli za Riwaq Al-Azhar katika vituo vya vijana.

Back to top button