Habari

Taasisi ya Masomo ya Kidiplomasia yaandaa kozi ya mafunzo kwa wanadiplomasia kutoka Nchi za Ulaya na Asia

Ali Mahmoud

0:00

Taasisi ya Masomo ya Kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya nje iliandaa kozi ya mafunzo katika uwanja wa kujenga uwezo wa kidiplomasia kwa kundi la wanadiplomasia kutoka nchi za Ulaya na Asia, kwa kushirikiana na Shirika la Misri la Ushirikiano kwa ajili ya maendeleo.

Taasisi ilifanya kozi hiyo, ambayo hutekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje kila mwaka katika muktadha wa mahusiano maarufu ya ushirikiano kati ya Misri na Nchi rafiki za Ulaya na Asia zinazojumuishwa na mpango huu, kwa ushiriki wa wanadiplomasia 28 kutoka Wizara za mambo ya nje katika nchi 14 nazo ni Bosnia na Herzegovina, Ukraine, Albania, Macedonia Kaskazini, Serbia, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Armenia, Mongolia, Nepal, Georgia, Uzbekistan na Azerbaijan.

Kozi hiyo, iliyofanyika kwa muda wa wiki mbili, ilishughulikia masuala kadhaa yenye kipaumbele ya kisiasa, usalama na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, na yanayohusiana pia na maendeleo katika Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati, pamoja na masuala kadhaa yanayohusiana na maendeleo ya ujuzi wa kidiplomasia katika nyanja kama vile mazungumzo, usimamizi wa migogoro, itifaki na sheria ya kimataifa, pamoja na seti ya mazoezi ya vitendo yaliyotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Kairo cha utatuzi wa migogoro, ulinzi na ujenzi wa amani.

Taasisi hiyo ilifanya sherehe ya kumalizia mwishoni mwa kozi ya mafunzo kuwaheshimu wanadiplomasia wa Ulaya na Asia wanaoshiriki, kwa mahudhurio ya Balozi Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya nje, Balozi Walid Hajjaj, Mkurugenzi wa Taasisi ya Masomo ya Kidiplomasia, pamoja na mabalozi walioidhinishwa mjini Kairo kwa nchi zilizoshiriki katika Kozi hiyo kupitia wanadiplomasia wake.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"