Vijana Na Michezo

ARUSHA WASICHANA WATANGULIA NUSU FAINALI KIKAPU

Timu ya Mpira wa Kikapu Wasichana kutoka mkoa wa Arusha imefanikiwa kuingia hatua inayofuata ya nusu fainali katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yanayofanyika kitaifa Mkoani Tabora.

Arusha imefikia hatua hiyo baada ya kuibuka mshindi dhidi ya Unguja katika mchezo wa robo fainali uliochezwa mapema saa 1 Asubuhi kwenye uwanja B wa shule ya Sekondari Tabora wavulana wavulana.

Mabingwa hao watetezi wamewafunga Unguja Vikapu 73-15, hivyo kuendelea na mbio za kutetea ubingwa wao waliouchukua kwenye UMISSETA 2022 baada ya kuwafunga Dar es salaam kwenye mchezo wa fainali.

Kwa upande wa Kikapu Wavulana uliochezwa sambamba na ule wa wasichana kwenye Uwanja A, Mabingwa watetezi Dar es salaam wamefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwashinda wenyeji Tabora kwa vikapu 86-25.

Dar es salaam ni moja ya Timu zinazopewa nafasi ya kubeba Ubingwa wa Kikapu mwaka huu, kutokana na ubora wa wachezaji wake huku timu za Pemba na Arusha pia zikipewa nafasi ya kusonga kwenye hatua zinazofuata.

زر الذهاب إلى الأعلى