Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA SEKTA YA BIMA NI MUHIMU KWA UCHUMI WA NCHI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema anatambua umuhimu wa mchango wa sekta ya bima kwa uchumi wa nchi na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo alipokutana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt.Baghayo Saqware na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amepongeza juhudi zinazofanywa na mamlaka hiyo kwa kuanzisha konsotia ya kilimo, pia nakuwataka kupanua wigo zaidi katika sekta za mifugo na uvuvi kwa kugusa wananchi wengi zaidi.

Naye, Kamishna Dkt.Saqware amewatambulisha Mabalozi wa Mamlaka hiyo kwa  Mhe.Rais akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Injinia Zena Ahmed Said, na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Wanu Hafidh Ameir na Mhe.Japhet Hasunga  ambao moja ya jukumu lao ni kutoa elimu ya uelewa wa Bima kwa wananchi.

Back to top button