Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA ELIMU NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa ilani ya Uchaguzi  ya CCM ya 2020-2025.

Ameyasema hayo leo alipoweka jiwe la msingi  wa ujenzi wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu  ya Mwalimu Nyerere, Kampasi ya Pemba eneo la Mtima Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuona umuhimu wa kufungua Kampasi hiyo kisiwani Pemba  ikiwa ni sehemu sahihi ya kusogeza huduma za jamii katika  sekta ya elimu kwa watu wa Pemba na Watanzania kwa ujumla.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi  alieleza kuwa mchango mkubwa wa Chuo hicho  kwa taifa na uzoefu waliokuwa nao   wa kutoa mafunzo kwa wahitimu walioiva kimaadili, kiuongozi , uadilifu, uzalendo na weledi wa hali ya juu ambazo ni nyezo muhimu kwa mtumishi yoyote anayepewa dhamana ya utumishi wa Umma.

Back to top button