Vijana Na MichezoWahusika Wamisri

Tariq Selim

 Tariq Selim alizaliwa katika mtaa wa Dokki mnamo Julai 15,1937 mwana wa Mohammed Selim na kaka mdogo wa Saleh Selim Rais wa kumi  wa klabu ya Al-Ahly.

Alijiunga na timu ya mpira wa miguu katika klabu ya Al-Ahly baada ya aligunduliwa na Hessein Kamel skauti maarufu halafu aliinuka katika timu za wachipukizi hadi kufikia timu ya kwanza mwaka 1954,kulingana na maagizo ya kocha Mokhtar Al-Tech.

Safari yake :

Marehemu alishiriki katika mechi yake ya kwanza kwa timu ya kwanza dhidi  ya timu ya Suez kwenye uwanja wa Suez, na alifunga mabao mawili katika mechi hii, na klabu ya Al-Ahly ilishinda 4/0.

 Na pia alishiriki katika kuhakikisha  mashindano 12 kwa klabu ya Al-Ahly, miongoni mwao ni  mashindano 7 ya ligi na mashindano matano ya kombe la Misri na pia ilishinda mashindano mawili na timu ya kitaifa, nayo ni kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1959, na mashindano ya Jamhuri ya kiarabu mwaka 1961/1962.

Alicheza kwenye  kiwango cha kimataifa kuanzia 1956 hadi 1963 ampabo alishiriki katika mashindano ya mataifa ya Afrika  1909,na  1963, na ligi ya Roma  ya Olimpiki mnamo 1960 na mashindano ya Mediterania   na kombe la Dunia la jeshi.

Alitangaza kustaafu kwake mwaka 1965, baada ya miaka 17 kwa shati la klabu ya Al-Ahly na kuelekea kufanya Kazi katika idara ya klabu ya Al-Ahly, halafu alirudia kwa Kazi yake ya asili  Kama mwanahewa , akawa mwanahewa mkubwa wakati wa Kazi yake katika kampuni ya kitaifa ya usafiri wa Anga.

Katika ugonjwa wake, alikuwa na hamu ya kuwepo katika mazoezi ya timu ya mpira wa miguu ili kuwasaidia wachezaji katika nyakati ngumu.

Na miongoni mwa misemo yake maarufu ni:

“Niko tayari kufanya Kazi Kama mlinzi kwenye lango la klabu ya Al-Ahly kwani huduma ya klabu ya Al-Ahly ni heshima kwangu,

Al-Ahly sio klabu ya michezo kwangu, lakini ni  nyumba yangu,  na hakuna mtu mmoja anayependa  kutoa siri  ya nyumba yake nje”.

Kifo chake :

Tariq Selim alifariki Dunia  Julai 16, 2016 akiwa na umri wa miaka  79 baada ya shida kubwa na ugonjwa, akiacha historia iliyojaa kutoa, uaminifu na ukweli  katika upendo wa klabu ya Al-Ahly kutuacha mwili wake, lakini kanuni yake na tabia yake zitabaki milele, ili kujifunza kutoka kwake vizazi wa kisasa na watakaokuja.

Back to top button