Dkt. Mostafa Madbouly akagua Banda la Soko la Hisa la Misri katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo
Rami El Dokani: Uwepo wa Soko la Hisa la Misri kwa mwaka wa nne mfululizo unalenga kuongeza viwango vya uhamasishaji wa uwekezaji wa wageni wanaotembelea Maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Soko la hisa: Kuandaa semina kuhusu kanuni na misingi ya kuwekeza katika soko la hisa kwa watazamaji wa maonyesho kwa ushiriki wa vyama vya kisekta.
Tunatafutia kuongeza viwango vya uelewa wa kifedha ili kuwawezesha wananchi kutambua fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia sadaka zinazotarajiwa sokoni.
Kairo ,Alhamisi tarehe 26 Januari 2023.
Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, akiwa ameambatana na baadhi ya mawaziri, alikagua banda la Soko la hisa la Kimisri wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 54 ya Vitabu ya Kimataifa ya Kairo, yaliyofanyika chini ya uangalizi wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kuanzia Januari 26 hadi Februari 6, pamoja na kauli mbiu “Misri – Twasoma – Twafikiri – Twaunda”.
Dk. Madbouly, alipokelewa na Rami El-Dokany, Mwenyekiti wa Soko la hisa la Misri, na hivyo kwa mahudhurio ya Dkt.Mohamed Farid Saleh , Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Fedha ya Misri, Ahmed Abdel Rahman, Makamu wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Fedha ya Misri, na kikundi cha viongozi wa Mamlaka na Soko la Misri.
Al-Dokani aliwasilisha kwa Waziri Mkuu malengo ya Soko la Hisa kutoka kushiriki katika kikao kipya cha maonesho hayo, pamoja na machapisho ya hivi punde ya kielimu yaliyotolewa na Soko la Hisa la Misri wakati wa shughuli za Maonesho ya Kitabu, navyo ni mfululizo ulioonyeshwa wa vidokezo muhimu zaidi vya kifedha na uwekezaji ambavyo lazima vijulikane na watu binafsi wanaotaka kufaidika na bidhaa na dhamana zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Misri kama njia ya kuwekeza na kuweka akiba.
Wakati wa ushiriki wake katika kikao cha 54 cha Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo, Soko la Hisa la Misri linaonesha idadi ya machapisho ya elimu yanayolingana na umri na makundi ya kijamii ya hadhira ya maonesho hayo, vijana kwa wazee, na pamoja na watu wenye uamuzi na uwezo maalum, wakati soko la hisa linapanga mashindano kadhaa kwa waanzilishi wa banda la kubadilishana hisa wakati wa siku za maonesho, na hii ni kwa ushirikiano na makampuni ya udalali na makampuni ya usimamizi wa mifuko, kwa lengo la kuhamasisha na kuongeza uelewa wa kifedha kwa wageni wa maonesho katika masharti muhimu zaidi ya kifedha na uwekezaji.
Katika muktadha unaohusiana na kando ya maonesho, Soko la Hisa la Misri litaandaa semina kwa umma kuhusu misingi na kanuni za uwekezaji katika dhamana na umuhimu wa Soko la Hisa la Misri kama jukwaa la uwekezaji na akiba kwa watu binafsi, na Jumatatu, Januari 30.