Taasisi ya “Maisha Bora” yaandaa warsha ya uhamasishaji katika Chuo cha ubaharia huko Alexandria kwa kutambulisha mradi wa kitaifa “Maisha Bora”
Mervet Sakr
Taasisi ya “Maisha Bora” iliandaa warsha ya uhamasishaji ndani ya makao makuu ya Chuo cha ubaharia katika mkoa wa Alexandria kwa lengo la kueneza utamaduni wa jumuiya na kazi ya kujitolea miongoni mwa vijana wa vyuo vikuu.
Bi. Nada Khader, Mkuu wa Mipango na Sekta ya Maendeleo Jumuishi katika Taasisi ya Maisha Bora, alishiriki katika kongamano hilo, Naye Dkt. Muhammad Massad, Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Uwandani katika Taasisi hiyo, Walizungumzia malengo ya mradi wa kitaifa, maisha yenye staha, shoka zake, na nafasi ya utendaji ya miradi ndani ya vijiji.
Kongamano hilo pia lilihusu kutambulisha kwa Taasisi ya “Maisha Bora”, kwa kuwa ndio mwavuli rasmi kwa vijana wa kujitolea katika mradi wa kitaifa, Maisha Bora, Pamoja na uwasilishaji wa mipango muhimu zaidi iliyozinduliwa na Taasisi.
Zaidi ya wanafunzi 400 kutoka Chuo Kikuu cha ubaharia walihudhuria kongamano hilo mbali na idadi ya washiriki wa kitivo cha chuo.
Ikumbukwe kuwa warsha hizo zinalenga kuongeza uelewa na kuanzisha mradi wa kitaifa wa maendeleo ya vijiji vya Misri “Maisha Bora” kwa vijana wa vyuo vikuu, na kuzitambulisha kwa juhudi za maendeleo zinazofanywa ardhini, sambamba na mwitikio wa Taasisi ya Maisha Bora kwa wito wa majadiliano ya kitaifa kwa taasisi za kiraia kufanya mazungumzo ya umma katika majimbo yote ya Jamhuri na makundi mbalimbali, na ndani ya juhudi za Muungano wa Kitaifa wa Kazi za Maendeleo ya Raia, taasisi inayokuja kama mmoja wa waanzilishi wake.