JUMLA ya walimu wa awali 179 wamepewa mafunzo kuhusu mbinu za kuwafundisha watoto wa elimu ya awali ili kuwezesha ujifunzaji wa mtoto kulingana na hatua za makuzi.
Akitoa mada kuhusu mbinu bora za ufundishaji kwa watoto wa elimu ya awali mkufunzi, Julia Kaita Mpunga amesema kuwa ili mtoto aweze kuelewa mwalimu anapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufundisha zitakazomsaidia mtoto kujiamini na kuwa mahiri katika masomo.
Anazitaja mbinu za kumsaidia mtoto wa elimu ya awali kuelewa kwa haraka kuwa ni michezo ambayo humsaidia kutenda zaidi, kufikiri, kujiamini na kunyoosha viungo.
Amesema mbinu nyingine ni hadidhi ambayo humsaidia kujua mambo mbalimbali ya zamani, kufurahisha, kufundisha na mbinu ya nyimbo ambazo humfanya mtoto kufurahi, kucheza, kujifunza lugha na kuhesabu.
Naye Lianda Fransis Mkufunzi kutoka Chuo cha Ualimu Butimba ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo kwa walimu wa elimu ya awali katika Chuo cha ualimu Bustani Kondoa amesema kuinua ufaulu kwa watoto hususani kwa ngazi ya elimu ya awali ambao ndio msingi katika kitovu cha elimu.
“Mtoto mdogo akielimushwa tunatarajia kuwa Taifa lililoelimika ndio maana Serikali inasisitiza matumizi ya mbinu bora za ufundishaji na jumuishi,” amesema Bi.Linda
Amesema mtumzi ya michezo humsaidia mtoto kukumbuka mafunzo aliyofundishwa darasani na humsaidia kukumbuka kile alichofundishwa darasani hivyo kutamsidia kujenga umahiri kwa mtoto.