Habari

Sheikh Al-Azhar asali sala ya Ijumaa katika kituo cha kiislamu alipowasili kwenye mji mkuu Bangkok

 

Kwenye sherehe kubwa kutoka kwa Waislamu nchini Thailand. Alipowasili katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, Mhe. Imamu Mkuu Prof. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kiislamu, alikuwa na hamu ya kwenda kwenye Kituo cha Kiislamu kufanya sala ya Ijumaa na umati wa waabudu, kubadilishana mazungumzo ya kirafiki na picha za kumbukumbu nao, na kuwasikiliza.

Umati wa waabudu, wakiongozwa na Imamu wa Msikiti wa Kituo cha Kiislamu na mhubiri wake katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, Shafii Abdul Qadir, waliandamana kuzunguka Imamu Mkuu, wakielezea furaha yao kubwa na ziara hii ya kihistoria ya Sheikh wa Al-Azhar, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kiislamu, kwa nchi yao.

Mhe. Imamu Mkuu aliwasili mchana huu katika mji mkuu wa Thailand Bangkok, ambayo ni kituo cha pili katika ziara yake ya kigeni huko Asia ya Kusini, kwa lengo la kuimarisha madaraja ya mawasiliano na Waislamu na kueneza maadili ya mazungumzo, uvumilivu na kuishi pamoja kwa binadamu.

زر الذهاب إلى الأعلى