Vijana Na Michezo

RAIS DK.MWINYI AHUDHURIA UFUNGUZI WA OLIMPIKI MAALUM BERLIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amehudhuria sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu mwaka 2023 katika uwanja wa Olimpia Jijini Berlin nchini Ujerumani jana tarehe 17 Juni 2023.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki katika michezo hiyo ikitafuta medali kwenye mpira wa wavu na riadha.
Rais Dk.Mwinyi katika msafara wake ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Pindi Chana, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dk.Abdallah Saleh Possi.
Mashindano hayo yamefunguliwa jana tarehe 17 Juni na kumalizika 25 Juni 2023.
زر الذهاب إلى الأعلى