Uchumi

Kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za uwekezaji na biashara kati ya Misri na Kenya

 

Balozi Wael Nasreddin Attia, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Kenya amekutana na Bi. Rebecca Miano, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya. Mkutano huo ulijadili njia za kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika nyanja za uwekezaji na biashara na kujiandaa kwa Kongamano la Biashara kati ya Misri na Kenya litakalofanyika pembezoni mwa kikao cha 7 cha kamati ya pamoja kati ya nchi hizo mbili jijini Nairobi chini ya uenyekiti wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili kuanzia tarehe 5 hadi 7 Machi 2024.

Wakati wa mkutano huo, waziri huyo wa Kenya alielezea nia ya nchi yake ya kupanua wigo wa ushirikiano na Misri kama mmoja wa washirika muhimu wa kibiashara wa Kenya, na kuvutia uwekezaji wa Misri kwenye nyanja mbalimbali, haswa ujenzi wa barabara, miundombinu, makazi, kilimo na umwagiliaji, afya na dawa, na uzalishaji wa umeme kutoka kwa rasilimali mbadala.

Nasr El-Din aliangazia nia ya Misri kuimarisha mahusiano ya ushirikiano na Kenya na kuhamisha utaalamu wa kampuni zake kwenye maeneo ya kipaumbele ya maendeleo kwa serikali ya Kenya, akisisitiza haja ya nchi za Afrika kutegemea uwezo wao wenyewe kuendeleza juhudi zao za maendeleo na kutoa kipaumbele kwa makampuni yao ya kitaifa katika kufaidika na fursa za kiuchumi zinazopatikana katika kila mmoja wao, pamoja na juhudi za kukuza biashara ya ndani ya kikanda.

زر الذهاب إلى الأعلى