Habari

Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Misri akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa NEPAD na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji

 

Kandoni mwa Kongamano la Aswan lililofanyika tarehe 2-3 Julai 2024, Balozi Ashraf Ibrahim, Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Misri, alikutana na Nardos Bekele Thomas, Mkurugenzi Mtendaji wa NEPAD. Mkataba wa maelewano kati ya pande hizo mbili na mpango kazi wa utekelezaji wa masharti yake ya kuanzisha shughuli za pamoja zinazolenga kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 na ajenda ya maendeleo ya Afrika 2063 katika nchi za bara hilo zilijadiliwa.

Kwa upande mwingine, walijadili haja ya kuhamasisha rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo Barani Afrika, na jukumu la Benki ya Maendeleo ya Afrika katika suala hili. Pande hizo mbili pia zilibadilishana maoni kuhusu jukumu muhimu lililotekelezwa na Umoja wa Afrika katika mchakato wa maendeleo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Balozi Ashraf Ibrahim pia alikutana na Balozi Jean Van Wetter, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Enabel, ambapo pande hizo mbili zilijadili njia za ushirikiano wa pamoja Barani Afrika, na kukagua uzoefu wa Shirika la Misri na Shirika la Ubelgiji katika kusaidia juhudi za maendeleo katika bara la Afrika. Pia walijadili uwezekano wa kufanya ushirikiano wa pande tatu kati ya mashirika hayo mawili katika maeneo ya kipaumbele kama vile elimu, afya, kilimo na umwagiliaji, katika baadhi ya nchi za Afrika kama vile nchi za Bonde la Mto Nile na nchi za Sahel na Sahara, ili kusaidia ndugu wa Afrika kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

زر الذهاب إلى الأعلى