Habari Tofauti

Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri akagua kazi za bwawa la “Julius Nyerere”

Mervet Sakr

Katika siku ya pili ya ziara yake katika nchi ndugu ya Tanzania.. Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji Dkt.Hani Sweilem amefanya ziara ya kikazi kwa eneo la bwawa la “Julius Nyerere” akiwa ameambatana na Balozi Sherif Ismail, Balozi wa Misri nchini Tanzania, na ujumbe wa kitaalamu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wawakilishi wa Ubalozi wa Misri nchini Tanzania,na muungano wa Misri unaohusika na utekelezaji wa bwawa hilo, mhandisi Ayman Attia na mhandisi Rafi Youssef, naibu mkurugenzi wa muungano huo.

Dkt. Swailem alisema kuwa mradi huu una umuhimu mkubwa kwa watu wa Tanzania, ambapo unalenga kuzalisha nishati ya umeme na kudhibiti mafuriko ya Mto Rufiji na kudhibiti uendelevu wa mtiririko wa maji yake, akibainisha kuwa kujazwa kwa ziwa la “Julius Nyerere” kulizinduliwa tarehe 22 Desemba 2022, katika sherehe kubwa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania alishiriki katika hilo.

Dkt.Swailem pia aliishukuru serikali ya Tanzania kwa imani kubwa iliyoiweka kwa makampuni ya Misri ili kutekeleza mradi huu mkubwa, na ushirikiano wa kujenga unaotolewa na mashirika ya serikali ya Tanzania na makampuni ya Misri.

Waziri alisifu utekelezaji wa mradi huu kupitia muungano wa Misri unaojumuisha Arab Contractors na kampuni ya El Sewedy Electric, inayothibitisha nguvu na tofauti ya makampuni ya Misri na inawakilisha uungaji mkono wa Misri kwa juhudi za maendeleo Barani Afrika, na maono yake ni kwamba maendeleo ya kweli ni kuanzisha miradi inayonufaisha nchi ndugu bila kukiuka haki za wengine au kusababisha madhara kwa nchi jirani.

Waziri wa Umwagiliaji pia alielezea fahari yake kubwa katika kiwango cha kimataifa makampuni ya Misri yaliyofikia katika kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu,ambapo makampuni ya Misri yalifanikiwa kutekeleza mradi huu mkubwa licha ya changamoto kubwa zilizokabili mchakato wa utekelezaji, na akibainisha kuwa mradi huu unachukuliwa kuwa mfano wa ushirikiano wa kikanda wenye kujenga kati ya nchi ndugu za Kiafrika kwa kuunga mkono juhudi za maendeleo na kufikia maslahi ya watu wao.


Dkt. Swailem alielezea matarajio yake ya kuendelea kwa kazi ya umoja huo katika miradi ya maendeleo sawa na kupanuliwa zaidi katika nchi za kiafrika, na hasa nchi za Bonde la Mto Nile, na kile kinachowakilisha ya mwelekeo wa kimkakati, akisisitiza hamu ya Misri ya kuimarisha ushirikiano na nchi za Bonde la Mto Nile na kwa kuendeleza maendeleo endelevu katika nchi zote za mabonde.

Katika ziara hiyo Dkt.Swailem alisikiliza kwa maelezo ya kina ya viongozi wa mradi kwa Kampuni ya Arab Contractors na Kampuni ya El Sewedy Electric kwa vipengele vya mradi huo, na maendeleo ya kazi yake na changamoto zilizokabili mchakato wa utekelezaji, ambapo ilielezwa kuwa urefu wa bwawa hilo ni mita 1025 kwa juu, urefu wa mita 131 na uwezo wa kuhifadhi takribani mita za ujazo bilioni 34, na Bwawa hilo linajumuisha kituo cha kuzalisha umeme kwa maji chenye uwezo wa megawati 2,115 kupitia mitambo 9, na Kituo hiki ndicho kikubwa zaidi nchini Tanzania kuzalisha umeme, na nishati inayozalishwa itasambazwa kupitia njia za kusambaza umeme za kV 400 hadi kwenye kituo kidogo cha umeme, ambapo nishati ya umeme inayozalishwa itaunganishwa na mtandao wa umeme wa kiumma.

Mradi huo pia unajumuisha ujenzi wa mabwawa (4) tanzu ya kuunda hifadhi ya maji, na mbali na njia ya maji kumwagika katikati ya bwawa kuu, na njia ya dharura ya kumwagika na handaki la mita 660 kuelekeza maji ya mto, na vichuguu 3 vya kupitisha maji vinavyohitajika kwa kituo cha nguvu, na daraja la kudumu la zege, na madaraja 2 ya muda juu ya Mto Rufiji, na eneo la mradi linahudumiwa kwa kujenga barabara za muda na barabara za kudumu ili kuwezesha harakati na kuunganisha vipengele vya mradi, gharama yake inayokadiriwa kuwa dola bilioni 2.90, na imepangwa kuwa bwawa hilo litaanza kuzalisha umeme baada ya kukamilika kwa mikingiko ya turbine zote na kuanza kwa kufanya kazi mnamo 2024.

زر الذهاب إلى الأعلى