Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje leo, Juni 17, 2023, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri imelaani shambulio la kigaidi lililolenga shule ya sekondari katika eneo la Mpondwe magharibi mwa Uganda, lililosababisha makumi ya vifo na majeruhiwa.
Misri imetoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Uganda na familia za wahanga wa shambulio hilo la kikatili, wakitakia kupona haraka kwa majeruhi.