Utambulisho Wa Kimisri

Chuo Kikuu cha Kairo

Mfumo wa kisasa wa elimu ulikuwa moja ya maendeleo muhimu zaidi nchini Misri mnamo nusu ya kwanza ya karne ya kumi na tisa, na ulihusishwa kikubwa na mradi wa kisiasa wa ufufuo ambao ulianzishwa na Muhammad Ali Pasha (1805-1848). Kabla ya Muhammad Ali Pasha kushikilia utawala wa Misri, Misri haijajua mfumo wa elimu kwa maana halisi, hakukuwa na chochote isipokuwa Al-Azhar na shule zingine zilizounganishwa na misikiti na madarasa katika miji na vijiji, lkn vyote havikuwa na mfumo wa pamoja unaovifanya viwe Muungano mmoja wa kielimu,pia vilikuwa mbali na utawala wa nchi na mfalme wake,ingawa viliweza kuwafundisha raia wa nchi kwa miongo kadhaa.

 Mfumo wa kisasa wa elimu uliwavutia wanafunzi wake kutoka madarasa na Al-Azhar mwanzoni mwake, kwa hivyo kulikuwa na kamati zilizokuwa zikizunguka nchi kutembelea madarasa na kuchagua wanafunzi bora zaidi kati ya wanafunzi wake kujiunga na shule za kisiasa. Wanafunzi hodari wa Al-Azhar pia walichaguliwa kujiunga na shule za juu wakati wa uanzishaji wake, lakini baadhi yao walibahatika kujiunga na ujumbe zilizopelekwa na Muhammad Ali kusoma. nchini Ufaransa

 Lakini utaratibu huo haukudumu kwa muda mrefu, basi mnamo 1841 makazi ya kimisri na Othmani yalikamilishwa kuweka mipaka kwa mradi wa kisiasa kulingana na ndoto za Muhammad Ali, kumaliza ukubwa wa jeshi, na kuanza kuingiza utawala wa nchi  katika kusimamia uchumi, kwa hivyo serikali haikuhitaji wafanyikazi zaidi, bali ilitoa idadi kubwa ya maaskari, maafisa na Halafu Muhammad Ali aliona haja ya kukagua mfumo wa elimu kulingana na hali mpya, kwa hivyo utaratibu mpya uliowekwa mnamo 1841 ambapo shule nyingi za msingi zilifutwa na idadi ya wanafunzi katika shule za kibinafsi ((juu)) ilipungua kulingana na hitaji la serikali kwa wahitimu wake na kwa kuongeza hii Mishahara ya wanafunzi imepunguzwa na kupangwa “Diwani ya Shule” kwa njia mpya.

  Kiunganishi hicho kati ya elimu ya kisasa na hitaji la serikali kwa wafanyikazi kinaelezea hali ya elimu mnamo enzi za Abbas Helmy wa kwanza (1848-1854) na Muhammad Saeed Pasha (1854-1863).

  Mnamo enzi ya Khedive Ismail (1863-1879), dhihirisho la utegemezi lilikamilishwa kwa kufungua mlango wa kukopa kutoka kwa taasisi za kifedha za Ulaya ikawa wazi kabisa, wakati Ismail alitaka kukamilisha miundombinu ya uchumi wa Misri ambayo babu yake Muhammad Ali alianza kwa kupanua miradi ya Umwagiliaji na kujenga reli, barabara, bandari ya Aleskandaria na miji mipya iliyo na mfereji wa Suez (Port Said na Ismailia) na upanuzi wa miji huko Kairo na Aleskandaria na hamu yake ya kuongeza nguvu ya jeshi la Misri kupanua kuwepo kwa Wamisri nchini Sudan, basi vyote hivyo vilihitaji pesa nyingi ambazo Ismail alikopa kutoka nyumba za kifedha za Ulaya. Kwa vyovyote vile, mpango wa mkopo wa Ismail ulikuwa ukikamilisha mchakato wa kuunganisha uchumi wa Misri katika uchumi wa Ulaya kwa uamuzi. Uzalishaji Maalum wa Kilimo ya Misri.

 

 Walakini, miradi ya kukamilisha miundombinu ya uchumi wa Misri na lengo la kuanzisha jeshi la kimisri liliifanya nchi hiyo katika enzi ya Khedive Ismail kuhitaji kuandaa makada wa kiutawala, kiufundi na kijeshi, wanaohitaji kufufuliwa kwa mfumo wa kisasa wa elimu uliofutwa na Abbas wa Kwanza na Muhammad Said Pasha.

 Wakati wa utawala wa Ismail, elimu ilipokea umakini mkubwa.Serikali ilianzisha shule na ilichukua gharama za kusoma, pamoja na gharama za maisha za wanafunzi, basi kurudisha tena (Diwani ya Shule), ambayo Saeed alikuwa ameifuta hapo awali, na bajeti ya elimu iliongezeka polepole. Serikali ilirudi kupeleka ujumbe huko Ulaya, kwa hivyo wengi wao walienda Ufaransa na idadi kadhaa za  shule za msingi zilianzishwa katika maeneo anuwai ya nchi kutoka Aleskandaria upande wa kaskazini hadi Minya kusini, na serikali ilisimamia madarasa (ofisi za kibinafsi), na shule zingine (za kati) na maalum (za juu) zilianzishwa, kwa hivyo (shule za Idara na Al Alsun) zilianzishwa mnamo 1868 (ambayo ilijulikana kama shule ya Sheria tangu 1886), Shule ya Umwagiliaji na Usanifu (inayojulikana kama Al-Mohandeskhana) mnamo 1866, Shule ya Dar Al-Uloom (mnamo 1872), ambayo ilianzishwa kuandaa walimu wa shule za msingi, Shule ya Nafasi na Uhasibu (mnamo 1868), Shule ya Kilimo (mnamo 1867) na Shule ya Ulimi mkale wa kimisri (Mambo ya Kale na Elimu za Misri) Mnamo 1869, shule maalum za jeshi ziliongezwa na vile vyote.

 Kwa msingi wa kuhifadhi shule za juu wakati wowote kuna mahitaji ya wahitimu wake na kupeana nao wakati wowote mahitaji yao ni machache, Shule ya Kilimo ilifungwa mnamo 1875 na Shule Ulimi mkale wa Misri ilifutwa mnamo 1876, baada ya kutoa  wataalam wa akiolojia ambao mmoja wao alibahatika awe kuwa mmoja wa waanzilishi wa uwanja huo huko Misri (Ahmed Kamal Pasha), wakati shule ya matibabu ilipokea umakini mkubwa

Wakati Mtaalam wa Misri Ali Pasha Mubarak aliposhikilia Diwani ya Shule mnamo 1868, alikusanya shule kadhaa za kibinafsi (za juu) huko Jumba la Darb Al-Jamamiz, basi aliweka kwa kila shule upande maalum huko Jumba na alianzisha maabara maalum kwa Kemia, Mazingira,na Maktaba kuu(Nyumba ya vitabu vya Khedewi)mnamo 1870, na uwanja mkubwa ambapo hutoa mihadhara ya maarifa tofauti kwa hivyo fursa ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Misri ilianza kuangaliwa,iwapo jambo hilo litasababisha  mawasiliano ya kisayansi kati ya maprofesa na wanafunzi, Kama jaribio hilo lingeendelea, lingekuwa kiini cha kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kwanza cha Misri.

Sera ya elimu iliendelea kulingana na uhusiano kati ya hitaji la serikali kwa wafanyikazi na upanuzi wa shule katika enzi zote za uvamizi wa Uingereza (1882-1922). Waingereza walizingatia madarasa bila kufanya juhudi za kuyaendeleza, wakati waliunganisha kukubaliwa kwa elimu ya msingi na hitaji la elimu ya sekondari na elimu ya juu, ili elimu ya msingi ipanuke kwa kiwango ambacho hitaji la shule za upili linatosha., Faragha (ya juu) ya wanafunzi wakati wa kufanya kazi ya kuboresha elimu hiyo na kuinua kiwango chake na hitaji la shule hizi kwa wanafunzi linahusiana na hitaji la serikali kwa makada wa kiutawala na kiufundi.Kuingia kwa shule kulikuwa kwa watoto wa wale ambao wanaweza kulipa karo . Hasa – iliyozuiliwa kwa jamii fulani ya kijamii baada ya uwezo na utayari wa kibinafsi zilikuwa vigezo vya kuchagua wanafunzi shuleni kabla ya enzi ya utawala wa Waingereza, kwani elimu ilikuwa bure ndani ya shule zote wakati wa Muhammad Ali na Ismail.

 Ilikuwa kawaida kwa mgao wa kifedha kwa Misafara ya elimu kupungua polepole hadi karibu ikasimame kabisa katika miaka kumi ya kwanza ya kazi hiyo, na ikiwa ujumbe uliendelea chini ya shinikizo la harakati ya kitaifa, idadi ya wajumbe ilipungua, bila kuzidi wanafunzi kumi, na wakati 1893 ambapo sera ya Ukoloni ya kielimu iliyoshikilia kutotekeleza serikali kuajiri  Wahitimu wa shule tofauti  ilipotangazwa, walipunguza mahitaji ya wanafunzi kujiandikisha katika shule za juu haswa, kwani ofisi ya maarifa iliamua idadi ya udahili kwa shule kwa kisingizio cha hofu ya kuongeza idadi ya wahitimu wasio na ajira na kuongeza karo za masomo katika shule za juu kufikia mwaka wa 1905 ili kupunguza mahitaji ya elimu ya juu na kuwapangia watoto mashuhuri peke yao na kisha Kufanya ajira katika utawala wa kimisri kumezuiliwa kwa wasomi wa kijamii wanaoshirikiana na kazi hiyo na kuwafukuza watu wa tabaka la kati, ambao kati yao msingi wa kuchukia ulowezi na kuwa na msingi wa  kazi ya kitaifa dhidi ya ukoloni.

Na ikiwa elimu ya juu ikawa kwa tabaka maalum tu, basi lazima iwe na mtindo wa Kiingereza ili kuunganisha sehemu hii ya kijamii na utamaduni wa Uingereza.Hivyo iliamuliwa mnamo 1898 kufanya elimu katika shule ya matibabu kwa lugha ya Kiingereza na sehemu ya Kifaransa ya Shule ya Walimu ilifutwa mnamo 1900 na idara ya Kiingereza ilianzishwa katika Shule ya Sheria mnamo 1899 ambayo masomo yanafundishwa kwa lugha hiyo Kiingereza kilianza kukua pole pole kwa gharama ya sehemu ya Kifaransa ya shule na ujumbe ulienda Uingereza baada ya kuelekea Ufaransa. Kwa hivyo, Uarabuni wa elimu ukawa hitaji la kimsingi la mahitaji ya harakati ya kitaifa. Wito wa Uarabuni ulifanikiwa kidogo. Tangu mwaka wa 1907, Uarabuni wa elimu katika Shule ya Sanaa na Ufundi na Shule ya Kilimo ilianza. Shule ya Sheria mnamo 1910 na elimu ya kibiashara ilianza katika ulimwengu wa Kiarabu.Uarabuni wa elimu katika shule za waalimu wa kiume na wa kike ulichelewesha hadi baada ya mapinduzi ya 1919, na wito wa Uarabuni ulishindwa katika shule za Muhandis Khana, Tiba, Duka la Dawa”Dispensari”,Tiba ya mifugo.

 Mwanzoni mwa karne ya ishirini, mapambano ya kitaifa dhidi ya uvamizi huo yalihusishwa na kupinga sera yake ya kielimu na mahitaji ya mfumo wa kitaifa wa elimu ambao utapanuka kuwajumuisha wale wanaotaka kutafuta maarifa kutoka kwa Wamisri na ndani ya mfumo wa harakati hiyo, wito wa kuanzishwa kwa “Chuo Kikuu cha Misri” ilikuwa baada ya Misri kuwa na msingi wa elimu ya juu.

Na miongoni mwa Shule muhimu zaidi za Misri ambazo zilikuwa kiini cha Chuo Kikuu cha Misri baadaye, kulingana na tarehe yake ya kuanzishwa : 

Shule ya Uhandisi

Shule ya Tiba

Shule ya Dawa

Shule ya Tiba ya Mifugo

Shule ya Kilimo

Shule ya Sheria

Shule ya Sayansi
Shule ya Biashara

شاهد أيضاً
إغلاق
زر الذهاب إلى الأعلى