Siasa

CCM yatangaza sekretarieti mpya

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) chini ya Mwenyekiti wake Dk Samia Suluhu Hassan imeteua wajumbe saba akiwemo Sophia Mjema ambae ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Mjema, anachukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka.

Pia, wajumbe wengine ni Daniel Chongolo ambae anaendelea na nafasi yake ya Katibu Mkuu, Anamringi Macha Naibu Katibu Mkuu Bara, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ni Said Mohamed

Wengine ni Dkt. Frank Haule ambae amekua Katibu wa Uchumi na Fedha, Mbarouk Nassor Mbarouk amekua Mkuu wa Idara ya Kimataifa na Issa Haji Gavu Mkuu wa Idara ya Organaizeisheni.

Aidha, wajumbe wa Kamati Kuuu Bara niMizengo Pinda, Hassan Wakasuvi naHalima Mamuya

 

زر الذهاب إلى الأعلى