Habari

Waziri wa Mambo ya Nje alikutana na Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Pembe ya Afrika

Nour Khalid

Mheshimiwa Bwana Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje alikutana na Hana Tita, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa haswa kwa Pembe ya Afrika , na hayo pembezoni mwa shughuli za kikao cha 42 cha Baraza la kiutendaji la Umoja wa Kiafrika, Siku ya Alhamisi, mwezi huu wa Februari tarehe 16 .

Na katika taarifa ya Balozi Ahmed Abo zayed, Msemaji rasmi na Mkurugenzi wa usimamizi wa Diplomasia ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje, akiashiria kuwa kikao hicho kimejumuisha masuala mbalimbali yanayohusiana na hali ya Amani na Usalama katika eneo la pembe ya Afrika, miongoni mwao yalikuwa ni hali nchini Somalia, ambapo Waziri Shoukry alisisitiza kuwa mahusiano ya nchi ya Misri na Somalia yanashuhudia mapya mengi, akielezea ziara ya mwisho wa Rais wa Somalia kwa Kairo mnamo Julai iliyopita, na maelewano ya pamoja ndani ya mfumo wa jukumu thabiti na la kihistoria la Misri katika kuunga mkono Somalia , pia inajumuisha msafara wa Umoja wa Afrika ya mpito nchini Somalia, ambapo pande hizo mbili zinakubalika umuhimu wa umoja wa washiriki wa mataifa ili kuunga mkono juhudi za utulivu wa hali nchini Somalia kupitia kutekeleza jukumu la ujumbe wa Umoja wa Afrika katika sura yake mpya ” ATMIS”.

Na Balozi Abo Zayed ameongeza kuwa kikao kilijumuisha pia maendeleo nchini Sudan, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje alisisitiza kuunga mkono kufikia maelewano kati ya vikosi vya kisiasa ya Sudan, yanayohakikisha kufanikiwa kipande cha mapitio na kufikisha matarajio ya raia wa Sudan katika kurejesha utulivu, na kuacha changamoto za awamu hii .

Na hiyo, kikao kilijumuisha suala la Bwawa la Al-Nahda, ambapo Waziri huyo alisisitiza tena mipaka ya msimamo thabiti wa Kimisri kwa umuhimu wa kufikia makubaliano ya lazimu juu ya sheria za kujaza na kuendesha Bwawa la Maendeleo, kwa kuzingatia masilahi ya nchi na kuhifadhi haki za maji za Misri.

Na msemaji rasmi alihitimisha taarifa zake kwa kudokeza maelezo ya Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa shukrani zake kwa juhudi za Misri za kuunga mkono utulivu katika Pembe ya Afrika , ambapo alithamini juhudi zote za Misri ili kuimarisha Usalama na Amani nchini Somalia na Sudan, akielezea nia yake katika mashauriano na uratibu endelevu na Misri katika suala hilo mnamo kipindi kijacho.

زر الذهاب إلى الأعلى