Utambulisho Wa Kimisri

Al-Azhar Al-Sharif kwa ufupi

Ahmed Hassan

Ulimi hauwezi kusema chochote na kalamu haiwezi kuandika neno moja hata wakati tunapozungumzia Taasisi za kale kama vile Al-Azhar, Inatosha kuiita kwa lakabu Al-Sharif,na katika Uislamu hakuna lolote lililoitwa hivyo ila liwe kuu, Kurani Tukufu na Al -Kaaba yenye heshima, pamoja na Al-Azhar Al Sharif.

Al-Azhar Al-Sharif ilianzishwa katika zama za Fatimid. Iliitwa hivyo kwa heshima ya  Fatima Zahra, Binti wa Mtume Muhammad ( S.W.A) , Na iliyojengwa wakati wa utawala wa Mu’izz Ladin Allah al-Fatimi , ambapo alimtegemea  Jawhar Al-Sakeli katika suala hilo, kuweka jiwe la msingi kwa mji wa Kairo pamoja na msikiti wa Al-Azhar mnamo mwaka wa 359 H, na shughuli hizo zimeendelea miaka miwili na sala ya  kwanza ya Ijumaa ilifanyika mnamo mwaka wa 360 H, Na ilianzishwa kwa kusala , kueneza mafundisho ya madhehebu ya Shia na kufundisha lugha na Sharia.

 Na iliendelea hadi zama za Ayyubid, lakini Saladin Ayubi alikuwa mwenye Sunnah na akaifunga AL-Azhar na  akubadilishwa na misikiti na shule nyingine ambapo Sayansi za Al-Azhar zilifundishwa, wanachuoni na wanafunzi wa Al Azhar walijifunza katika shule hizo, kwa hivyo mchango wake umeendelea, kisha ikafunguliwa na Baybars wakati wa Mamluk (zama za Mamllik) kwa mafundisho ya Ahl al-Sunnah na Jama’ah, na kuendelea na jukumu lake la elimu, kujifunza Sayansi za lugha, Sayansi ya Sharia, falsafa na mantiki.

Ni ya kutosha kwamba mnamo kipindi hiki AL-Azhar iliendeleza urithi wa Kiarabu na kiislamu kwa ujumla baada ya kuanguka Dola la Baghdad na Al-Andalusia. Wanasayansi wa nchi hizo kwa wakati huo hawakuona kuwa kimbilio chao ila Al-Azhar. Watawala wa Mamluk waliwakaribisha na kuwapa pesa na kuwawezesha kufundisha katika Msikiti wa Al-Azhar. Jukumu lake liliendelea hata katika Dola la Ottoman mpaka wakati wa sasa, Wakati kampeni ya Ufaransa ilipoanzishwa, wasomi wa Al-Azhar waliongoza upinzani na kisha wakashiriki katika Maendeleo, yaliyoanzishwa na Muhammad Ali, na waliongoza kuchapisha na kufanya kazi katika magazeti. Jukumu la Imamu Muhammad Abdo linatosha wakati alipokuwa akiongoza magazeti ya Misri, na walisafiri katika Ujumbe wa kisayansi, na wanashiriki katika ujumbe wa kwanza, na imamu wao alikuwa ni Rafaa al-Tahtawi, aliyeeleza kila kitu alichokiona huko Paris  Katika kitabu chake (Talkhis El Ibriz Fi Tashkhis Pariz), na walifanya kazi katika shule zilizoanzishwa na Muhammad Ali katika kila uwanja unaofaidika  lugha hiyo, na wale ambao hawakujifunza Al-Azhar kuchukuliwa kutoka kwa wanasayansi wake. Walichangia maendeleo ya kisayansi: Falaki, Hisabati, Tiba, na Sayansi mbalimbali.

 Miongoni mwa Sayansi zilizofundishwa katika Al-Azhar ni ujumbe wa Sheikh Al-Damanhuri (Ain al-Hayat Fi Estinbat El Meyah), na pia (Al Kawl Al Sarih Fi Elm El Tashrih)  Jabrati pia alijifunza Falaki,alikuwa Mtaalamu katika Hisabati,na alizingatia  Historia.

Sasa Al-Azhar ni marejeo  ya Sunni kwa Waislamu wote Duniani kote.. Inahangaika kueneza Usawa na Wastani, hufundisha wanafunzi wake kwa Fikhi ya madhahabu na maoni mbalimbali madamu madhahabu hizo ni sahihi , hata Al-Azhar inafundisha madhahabu tofauti, mafundisho na maoni ya uongo katika mafundisho ya Imani ( mada ya Akiida );ili kutoa majibu juu yake kwa Dalili na Akili.

Jukumu la Al-Azhar limedhahirisha wazi katika Ulimwengu wa Kiislamu, haswa Barani Afrika, ambapo Al-Azhar ilianzisha kitengo cha kufundisha lugha za Kiafrika, fasihi pamoja na sayansi za Kiislamu kwa lugha hizo mnamo 1967, pia kuanzishwa kituo cha tafsiri ya vitabu vya Kiislamu kwa lugha hizo,pia kuanzisha Kituo cha Uchunguzi cha Al-Azhar kwa kupambana na mawazo makali na mawazo ya harakati na vikundi vya ugaidi katika bara zima . Pamoja na kupeleka ujumbe wa Kiislamu kueneza mafundisho ya dini ya Kiislamu, na dhana sahihi na kufundisha sayansi ya lugha na sheria ya Kiislamu kikweli.

 Al-Azhar pia hupokea wanafunzi waafrika kujifunza ndani yake, iwe katika taasisi zake na chuo kikuu chake . Jamii ya Kiafrika ni jumuiya kubwa zaidi ya wanafunzi katika Al-Azhar.

Imamu mkuu Sheikh wa Al-Azhar, Dkt. Ahmed Al-Tayeb, ametoa maelekezo ya kuongeza idadi ya Ujumbe kwa nchi za Afrika na Idadi ya Udhamini uliotolewa kwa wanafunzi wa Afrika.

Mwenyezi Mungu alinde Misri na Al-Azhar yake sawa ni Msikiti na Chuo Kikuu.

شاهد أيضاً
إغلاق
زر الذهاب إلى الأعلى