Waziri wa Misri wa Al-Awqaf ashiriki katika shughuli za Mkutano wa Tatu wa Afrika wa kukuza Amani nchini Mauritania
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Al-Awqaf, alifanya ziara kwa muda wa siku 3 nchini Mauritania; kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa Afrika wa kukuza Amani, uliofanyika Mwaka huu chini ya kichwa “Saidieni wote kwa Amani ” kwa maandalizi ya kongamano la Amani la Abu Dhabi.
Mheshimiwa Waziri wa Al-Awqaf, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nouakchott, alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Kiislamu na Elimu asili ya Mauritania, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Pamoja na Balozi Khaled Youssef, Balozi wa Misri kwa Mauritania, na wafanyakazi wa Ubalozi.
Ziara ya Mheshimiwa Waziri wa Misri wa Al-Awqaf ilishuhudia shughuli nyingi, ambapo Mheshimiwa Waziri alishiriki kama mzungumzaji mkuu katika kikao cha ufunguzi wa mkutano, ambacho kilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya kidugu ya Kiislamu ya Mauritania, Rais wa Nigeria, Naibu Waziri mkuu wa Guinea-Bissau na Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu. Katika hotuba yake, Waziri wa Al-Awqaf alisisitizia umuhimu wa kufanya kazi kuimarisha misingi ya uraia sawa katika suala la haki na wajibu kwa misingi ya kibinadamu na kitaifa, imani katika utofauti na heshima kwa tofauti ya kila aina.
Kwa upande mwingine, Waziri wa Al-Awqaf alishiriki katika semina, iliyotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya Mauritania kwa ushiriki wa Katibu Mkuu wa Chuo cha Fiqh cha Kiislamu cha Sudan, Sheikh Adel Hassan Hamza, na Waziri wa Zamani wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania, Abu Bakr Ould Ahmed.
Balozi wa Misri alifanya karamu ya chakula cha jioni kwa heshima ya waziri wa Al-Awqaf, ambapo walioshiriki ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Fatwa na malalamiko wa Mauritania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Kiislamu na Elimu Asilia ya Mauritania, mabalozi kadhaa wa Kiarabu walioidhinishwa nchini Mauritania, alama za Jamii ya Misri na wawakilishi wa kampuni za Misri zinazofanya kazi nchini Mauritania, ambapo aliwapa vitabu kadhaa vilivyotolewa na Wizara ya Al-Awqaf.