Habari

RAIS DK.MWINYI AZIHIMIZA TAASISI KUWASILISHA MICHANGO ZSSF

0:00

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amezitaka Taasisi za Serikali na jumuiya zote za waajiri na waajiriwa wahakikishe wanawasilisha michango  katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji wa mfuko huo katika kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao wanapostaafu na kuhitaji mafao yao.

Ameyasema hayo leo  katika kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kuzindua mradi wa Mji wa Dk.Hussein Ali Mwinyi  uliopo Mombasa Zanzibar  pamoja na Mfumo wa huduma kwa wateja wa  kuwasiliana wa ZSSF WhatsApp ukumbi wa Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha , Rais Dk.Mwinyi amewashauri  wajasiriamali wote wajisajili na kuchangia Mfuko wa Hiari kupitia mfuko huo kwani una faida kubwa kwa biashara zao .

Vilevile, amewapongeza ZSSF kwa kuanza kulipa mafao mapya mawili kwa wanachama wake waliopoteza ajira na walioumia wakiwa kazini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewapongeza ZSSF  kwa kuzingatia utekelezaji wa agizo lake alilolitoa siku ya Wafanyakazi mei mosi mwaka 2023 kuongezeka kwa malipo ya pensheni   kwa  wastaafu.

Back to top button