RAIS DKT.MWINYI AHIMIZA AMANI, MARIDHIANO, MSHIKAMANO KWA WAZANZIBARI AKEMEA UPOTOSHAJI KWA UMMA
Ahmed Hassan
Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wananchi kushiriki katika mikutano ya vyama vya siasa inayoendelea Zanzibar bila ya uvunjifu wa amani na kuwahimiza wazungumzaji wa mikutano hiyo kuhubiri amani, utulivu, mshikamano na maridhiano.
Demokrasia inataka kushauriana yaani (Constructive Criticism) kueleza mambo ya kujenga na sio kuzusha au kueleza mambo yasiyo na uhalisia ili kuupotosha umma.
Dkt. Mwinyi amesema changamoto ya Bandari ya Malindi inasababishwa na jambo moja kuu ambalo ni kuwa na gati moja dogo la kushushia mizigo ambalo linasababisha foleni za meli kushusha hadi siku 7, hata hivyo alieleza kuwa utatuzi wa changamoto hiyo ni kuwa na bandari kubwa zaidi na gati nyingi zenye vifaa vya kisasa hata hivyo Serikali imechukua hatua ya kuagiza zana mpya ambazo tayari zimeanza kutumika ili kupunguza muda wa ushushaji mizigo bandarini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar leo tarehe 28 Februari 2023.