Habari
Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania inatambua na kuheshimu usawa wa kijinsia
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania inatambua na kuheshimu usawa wa kijinsia kwa kuona umuhimu wa kuwachagua wanawake kwenye mihimili yote Serikalini.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na uongozi wa Taasisi ya kiraia inayounganisha Jumuiya za wanawake kutoka vyama mbalimbali vya siasa vyenye usajili kamili nchini, Taasisi ya Sauti ya wanawake wenye ulemavu (SWAUTA), Chama cha wabunge wanawake (TWPG) na Umoja wa wanawake wa Baraza la Wawakili (UWAWAZA). T-WCP – ULINGO. Waliofika Ikulu, Zanzibar kumkabidhi tuzo ya hongera kwa mafaniko ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
Amesema Serikali zote mbili zitaendelea kutoa fursa kwa wanawake katika maeneo mbalimbali ili kutekeleza azma yao kufikia 50 kwa 50.
Rais Dk. Mwinyi pia amewapongeza ULINGO kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa hatua ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa bila kujali tofauti ya itikadi zao za kisiasa pamoja na kuwashirikisha wanawake wengi na kuwashajihisha kitaaluma kujua haki na wajibu wao kwenye masuala haki na siasa.