Umoja wa Mataifa uliamua kutenga Julai 7 ya kila mwaka kuadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili Duniani, kwa kuimarisha matumizi yake ya Umoja na Amani, kukuza utofauti wa Utamaduni, na kutengeneza Ufahamu na kuimarisha mazungumzo kati ya ustaarabu kwa namna inavyoimarisha Umoja katika utofauti na uelewano wa kimataifa, na uvumilivu tena mazungumzo.
Kiswahili ni lugha rasmi nchini Tanzania, Kenya, Uganda, vilevile ni mojawapo ya lugha za kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, pamoja na Rwanda na Burundi.
Aidha, ni miongoni mwa lugha zilizoidhinishwa na Umoja wa Afrika, vilevile Jumuiya ya Afrika Mashariki yaizingatia lugha rasmi ya mawasiliano ya pamoja.
Ikumbukwe kwamba Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani kwa kauli mbiu ya ” Kiswahili kwa ajili ya Amani na Ustawi” mbapo kuna zaidi ya wazungumzaji milioni 200 wa lugha ya Kiswahili, ikiwa ni mojawapo ya lugha za kiafrika zinazozungumzwa zaidi, na inajumuisha zaidi ya lahaja kuu 15.
Mnamo 1950, Umoja wa Mataifa ulichukua hatua ya kuanzisha kitengo cha lugha ya Kiswahili, na hivi sasa lugha ya kiswahili inajitokeza kuwa mojawapo lugha za kiafrika zenye umuhimu zaidi katika uwanja wa mawasiliano ya kimataifa.
Kwa muktadha huo, tarehe saba mwezi wa Julai imetangazwa kama Siku ya Kiswahili Duniani, nayo ni lugha ya kwanza ya kiafrika inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa kwa namna hiyo Maalumu.