Habari

Rais El-Sisi ampokea Teresa Evoa Assanjonou, Mwenyekiti wa Seneti ya Jamhuri ya Guinea ya Ikweta

Mervet Sakr

0:00

Alhamisi Septemba14, Rais Abdel Fattah El-Sisi amempokea Bi.Teresa Evoa Assanjonou, Mwenyekiti Seneti ya Jamhuri ya Guinea ya Ikweta, kwa mahudhurio ya Mshauri Abdel Wahab Abdel Razek, Mwenyekiti wa Seneti, na Mheshimiwa Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje.

Msemaji wa Ofisi ya Rais wa Misri, Mshauri Ahmed Fahmy, alisema kuwa Rais aliomba kufikisha salamu zake kwa Rais Teodoro Obiang, akisifu mahusiano ya nchi mbili kati ya Misri na nchi ndugu Guinea, na kuonesha nia ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, iwe katika ngazi za nchi mbili au bara, haswa kuhusiana na kukuza biashara na uwekezaji wa ndani ya Afrika, na kudumisha amani na usalama wa bara.

Kwa upande wake, Rais wa Seneti ya Guinea ya Ikweta alitoa ujumbe wa maandishi kwa Rais Obiang, ambao ni pamoja na kuonesha shukrani kubwa kwa Misri na uongozi wa Misri, kuthamini maendeleo endelevu mnamo kipindi cha uhusiano wa nchi mbili kati ya nchi hizo mbili, na kutarajia kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika ngazi mbalimbali, kwa kuzingatia juhudi za Misri za kukidhi matarajio ya watu wa Afrika kuelekea utulivu, maendeleo na ustawi, na mchango wake mzuri katika kuendeleza hatua za pamoja za Afrika.

Mkutano huo ulijadili njia za kuimarisha matarajio ya mahusiano ya nchi mbili, haswa katika ngazi ya Bunge, pamoja na kuimarisha uwekezaji wa Misri katika Guinea ya Ikweta, kuboresha masharti ya biashara kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kusaidia maendeleo na ujenzi wa uwezo na makada wa ndugu katika Guinea ya Ikweta katika sekta mbalimbali.

Back to top button