Habari

Rais El-Sisi akutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz

Tasneem Muhammad

0:00

Jumapili Septemba10, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, pembezoni mwa mkutano wa G20 nchini India.

Mshauri Ahmed Fahmy, Msemaji rasmi wa Urais wa Misri, alisema kuwa viongozi hao wawili walisifu maendeleo ya mahusiano ya nchi hizo mbili kati ya Misri na Ujerumani katika nyanja zote, zilizooneshwa kwa kiwango cha kubadilishana ziara kati ya viongozi waandamizi wa nchi hizo mbili katika miaka iliyopita, akisisitiza hamu ya kuongeza ushirikiano wa pamoja mnamo kipindi kijacho na kuimarisha uratibu na mashauriano ya kisiasa.

Pande hizo mbili pia zilipitia mifumo ya ushirikiano iliyopo katika nyanja mbalimbali, haswa katika sekta za uchukuzi, viwanda na nishati, pamoja na kufanya kazi ili kuongeza uwekezaji wa Ujerumani nchini Misri na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili.

Msemaji huyo aliongeza kuwa mkutano huo pia uligusia njia za kuratibu juhudi kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa kupambana na uhamiaji haramu, pamoja na maendeleo ya masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa ya maslahi ya pamoja, ambayo ni mgogoro wa Sudan, pamoja na mgogoro wa Urusi na Ukraine.

Back to top button