MWINYI AMESEMA UMOJA KWA WANA CCM NI USHINDI
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kwamba umoja miongoni mwa wanachama wa CCM ni muhimu katika kupata ushindi wa kushika dola. Amelaani wanachama wanaoleta viashiria vya makundi ndani ya chama.
Dk.Mwinyi ameelekeza kuanza mafunzo kwa Viongozi wa CCM ngazi zote, kuingiza wanachama wapya, wanachama kujiunga na CCM na kuhamasisha wananchi waliotimiza miaka 18 kujiandikisha katika daftari la Wakaazi.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa Serikali kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi. Amegusia pia suala la uchumi ndani ya chama, akisisitiza umuhimu wa kutumia rasimali zilizopo kwa kuongeza vipato na kuepuka hali ya chama kuwa ombaomba. Akihimiza vikao vya chama kufanyika kikatiba kwa ngazi zote, ameelekeza Sekretarieti ya CCM kusimamia hilo.
Ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Amani Mkoa, Wilaya ya Mjini, Unguja.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Dk. Hussein Ali Mwinyi za kukiimarisha chama, ambapo anatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na CCM. Aidha, ziara yake inajumuisha mikutano ya ndani na mazungumzo na viongozi wa CCM, Mabalozi, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri za CCM kutoka