Habari

KAMILISHENI TARATIBU ZA UMILIKI WA ENEO LILIPO JENGO LA KITEGA UCHUMI KANGE ILI LIANZE KUFANYA KAZI – KAMATI YA LAAC

0:00

 

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka Halmashauri ya Jiji la Tanga kukamilisha taratibu za umiliki wa eneo walilojenga mradi wa jengo la Kitega uchumi katika stendi ya Kange ili mradi huo uanze kufanya kazi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Halima Mdee (Mb) akizungumza Machi 25, 2024 wakati wa majumuisho akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, mkoani Tanga.

Mhe. Mdee amesema Serikali imeweka fedha nyingi katika mradi wa eneo la Machinga na Jengo la Kitega Uchumi ndipo alipowataka uongozi wa Jiji la Tanga kufanyia kazi kwa haraka kwa kuwalipa fidia wananchi wa eneo walilowekeza miradi hiyo ili Halmashauri ya Jiji la Tanga liwe na umiliki wa eneo hilo.

Aidha, Mhe. Mdee amawataka watendaji wote wa Halmashauri ya jiji hilo kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Sheria, Kanuni na Taratibu kwani kwa kufanya hivyo watendaji hao wataisadia Serikali kuondokana na hasara lakini pia kuondoa migogoro baina yao na wananchi.

“utamaduni wa Kamati ya LAAC itamfuata mtu popote alipo atakaesababisha, kuipa hasara Serikali hizi ni fedha za umma. Alisema Mdee.

Pamoja na kusisitiza kusimamiwa kwa haraka mradi wa machinga complex ukamilike kwa haraka ili thamani ya fedha ionekane, Mhe. Mdee ameutaka uongozi wa Jiji la Tanga kuangalia namna ya kuweka mazingira mazuri ya stendi ndogo ndogo zilizopo katika maeneo tofauti ya Jiji hilo kutokuathiri ufanisi wa kazi wa stendi kubwa iliyopo Kange.

Back to top button