Habari
Waziri Mkuu atembelea na kukagua miundombinu na vifaa tiba vyake
Muonekano wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, Mtwara ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 07, 2023 ametembelea na kukagua miundombinu na vifaa tiba vyake.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, Mtwara kuwa mkombozi kwa Wanakusini na nchi jirani ili wananchi wasiende umbali mrefu kupata huduma badala yake huduma zote ziishie hapo.
Amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na vifaa tiba vya kisasa kwenye maeneo yote ya utoaji wa huduma za afya.