Habari Tofauti

Shirika la Feed the Future Kilimo Tija  Tanzania limeandaa mafunzo ya mbinu za bora za uzalishaji wa kilimo

0:00

Shirika la Feed the Future Kilimo Tija  Tanzania limeandaa mafunzo ya mbinu za bora za uzalishaji wa kilimo cha mboga mboga na matunda kwa mabwana shamba wa serikali mkoani Njombe.

 Mafunzo hayo kwa mabwana shamba yanalenga kuwaongezea ujuzi maafisa ugani wa serikali ili  waweze kutoa elimu ya matumizi ya mbinu bora za kilimo kwa wakulima wa mbogamboga na matunda.

Daktari wa mifugo Masalu Mroje  kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Njombe wakati akifungua mafunzo hayo amewaomba maafisa ugani wanaoshiriki mafunzo hayo kuwa wasikivu katika ili waweze kuyatumia kwa vitendo katika kuwahamasisha wananchi kulima kitaalamu ili kupata tija.

Naye Bwana shamba mwandamizi kutoka Shirika la Feed the Future Kilimo Tija Tanzania Ayubu Metelei amesema lengo la mradi huo nikuhakikisha vijana na akina mama wanajikwamua  kiuchumi kupitia kilimo kwa kutumia teknolojia na mbinu bora za kilimo hasa kwenye kilimo cha mboga mboga na matunda.

Jumla ya Mabwana shamba 20 kutoka Halmashauri ya Mji Njombe ,Halmashauri ya Mji Makambako,Halmashauri ya wilaya ya Njombe na Halmashauri ya wilaya Wangingombe wanashiriki mafunzo hayo kwa nadharia na vitendo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe  kuanzia  Julai 25,2023 hadi Julai 28,2023.

Back to top button