Habari

El-Sisi aagiza kuongeza Tuzo za Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu kufikia karibu Paundi milioni 2

Ali Mahmoud

0:00

Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana, Jumamosi, na Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri mkuu, Dkt. Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Al-Awqaf, na Bi. Nevin Al-Qabbaj, Waziri wa Mshikamano wa Jamii.

Msemaji rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia “kufuatilia utetezi na shughuli za jamii za Wizara ya Awqaf”.

Mheshimiwa Rais aliagiza kuendeleza mpango jumuishi wa uanzishaji wa misikiti inayohusishwa na Wizara ya Al-Awqaf katika ngazi ya mikoa yote ya Jamhuri, ijumuishe shughuli zote za utetezi na usomaji wa Qurani Tukufu, na nguzo ya usambazaji wa ukweli wa Dini katika Jamhuri yote, kwa kuzingatia uteuzi sahihi wa maeneo yao na ugawaji wa nafasi inayofaa kwao, pamoja na kuongeza ufanisi wa misikiti mikuu katika kila mkoa.

Kukamilisha juhudi za serikali kueneza hotuba ya wastani ya Dini halisi na kuimarisha misingi yake thabiti, ambazo ilisikika zaidi ya upeo wa ndani wa Misri, Waziri wa Al-Awqaf alipitia juhudi za Wizara kupitia kozi za mafunzo kwa baadhi ya maimamu, wahubiri na viongozi wa kidini Barani Afrika, kwa lengo la kueneza utamaduni wa lugha ya mazungumzo, imani ya utofauti na kukubalika kwa wengine.

Waziri wa Al-Awqaf alionesha maendeleo ya hivi karibuni ya programu iliyoendelezwa kwa ajili ya mafunzo ya maimamu wapya na matokeo ya mashindano ya uteuzi wao wa kuchagua watu bora kutoka mtazamo wa kisayansi na kiutamaduni, ambapo Mheshimiwa Rais aliagiza kuimarisha programu za mafunzo kwa maimamu, kwa njia ambayo inachangia usafishaji wa utu wa maimamu na mawazo yao ya da’wah na ya kiutamaduni kwa njia ya kisasa ambayo inawasaidia kuunda maono ya kweli katika mfumo wa kiakili ulio wazi.

Msemaji rasmi huyo aliongeza kuwa Mheshimiwa Rais aliagiza kwa kuongeza Tuzo za mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu kufikia karibu Paundi milioni 2, yatakayoandaliwa na Wizara ya Al-Awqaf kupitia mwezi ujao kwa ushiriki mpana wa nchi mbalimbali za Dunia, inayoshughulikia kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kuelewa maana na madhumuni yake kwa wale wenye sauti nzuri.

Mpango wa Wizara ya Al-Awqaf wa kujiandaa kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika ngazi za kidini na kijamii pia uliwasilishwa na hili kupitia kuongeza shughuli za utetezi na kusoma Qurani Tukufu wakati wa Mwezi Mtukufu, pamoja na mchango wa wizara katika huduma za jamii kupitia miradi ya jamii kama vile hati ya dhabihu, kulisha na kusambaza bidhaa za chakula kwa familia zilizo hatarini zaidi, kwa ushirikiano na uratibu na Wizara za Mshikamano wa Kijamii na Ugavi na mamlaka za serikali za mitaa katika ngazi ya mikoa ya Jamhuri.

Waziri wa Al-Awqaf pia alipitia juhudi za wizara katika uwanja wa Tafsiri na Uchapishaji, haswa tafsiri ya hivi karibuni ya maana ya Qurani Tukufu katika idadi mpya ya lugha, ambazo zitazinduliwa wakati wa kikao kijacho cha Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo, kwa lengo la kueneza Uislamu wa kweli kuhusu tafsiri ya maana ya Qurani Tukufu mbali na upotoshaji wowote au utiaji chumvi, katika mwanga wa mkakati wa serikali wa kueneza mawazo yaliyomilikiwa wastani.

Pia, Mheshimiwa Rais alifuata shughuli za Mamlaka ya Al-Awqaf na juhudi za maendeleo yake, ambazo zilionekana katika ongezeko endelevu la mapato yake, ambapo mapato yake mnamo Mwaka wa 2022 yaliongezeka hadi karibu Paundi bilioni 2 ikilinganishwa na karibu Paundi milioni 600 mnamo mwaka wa 2014.

Back to top button