Balozi wa Misri akutana na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini
Mervet Sakr
Balozi Moataz Mustafa Abdel Qader, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Sudan Kusini, amekutana na Balozi Deng Daoding, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Nchi ya Sudan Kusini, ikiwa ni sehemu ya kufuatilia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukry nchini Sudan Kusini Mei 9, 2023.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, Balozi Deng Dao, ameelezea shukrani zake na kufurahishwa na ziara muhimu ya Waziri wa Mambo ya Nje mnamo Mei 9 2023, akishukuru ujumbe uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah Al-Sisi, kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, juu ya maendeleo katika Jamhuri ya Sudan, pamoja na njia za kuimarisha uhusiano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande wake, Balozi Moataz Mustafa Abdel Qader alisisitiza nguvu na kina ya mahusiano kati ya viongozi na watu wa nchi hizo mbili, na nia ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuendelea kuunga mkono na juhudi za kutoa msaada kwa Sudan Kusini katika sekta na nyanja mbalimbali, na kuimarisha mashauriano na uratibu kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya kikanda ya wasiwasi wa pamoja, ambayo ni mgogoro wa Sudan na athari zake kwa nchi hizo mbili kama majirani wa moja kwa moja wa Sudan.