Habari

“Waziri wa Uhamiaji”: milango yetu iko wazi kwa mapendekezo yote ya Wamisri nje ya nchi

Ali Mahmoud

Balozi Soha Gendi, Waziri wa nchi kwa Uhamiaji na masuala ya Wamisri nje ya nchi, alipokea Alaa Aref, mmoja wa wana wa Jamii ya Misri nchini Romania, mkurugenzi wa kikanda wa Shirika la ndege la kiromania “Tarum”, na wakili wa mauzo ya kampuni ya kiromania na mwakilishi wake nchini Misri, kujadili njia za ushirikiano wa kuwahudumia wana wa Jamii ya Misri nchini Romania na nchi jirani.

Waziri wa Uhamiaji alikaribisha ushirikiano na kampuni mbalimbali za kimataifa zinazofanya kazi kwa manufaa ya Wamisri popote walipo nje ya nchi, na kuchunguza mapendekezo yao, akisisitiza kuwa wana wetu nje ya nchi wanazingatiwa kama sehemu ya nguvu laini, na wana uangalifu wa kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali kutoa njia zote zinazowezekana za kufaidika.

Waziri huyo alisisitiza nia yake ya kufungua mlango kwa wote na kusikiliza maoni anuwai na kuchunguza uwezekano wa kuyafikia, kulingana na malengo ya serikali kufikia maendeleo endelevu, akisifu ushirikiano wa awali wa Misri na uhuru wake na shirika la ndege la kiromania “Tarum” katika kuendesha daraja la hewa kuwaokoa wana wetu wamisri waliokwama Romania wakati wa Janga la Corona na baadaye kukimbia vita vya Ukraine -Urusi.

Alaa Aref, mmoja wa wana wa jamii ya Misri nchini Romania na mkurugenzi wa kikanda wa shirika la ndege la kiromania “Tarum”, mwakilishi wake na wakili wa mauzo yake nchini Misri, alieleza kuwa kampuni hiyo inatoa safari tatu za ndege za kawaida za kila wiki kwa miji ya Sharm El-Sheikh na Hurghada na jumla ya safari 12 nchini Misri, na pia inafanya kazi kama njia ya usafiri kati ya Misri na nchi kadhaa za Ulaya Mashariki.

Tarum pia inatarajia kufanya safari mbili za kila wiki za kawaida, kwa upatani, kati ya Misri na Romania kuanzia Aprili 1 ijayo kwa sambamba na sikukuu za ufufuo na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambalo linatoa nafasi kwa wanafunzi na wamisri nje ya nchi katika Romania na karibu nayo kunufaika na maonesho yake mbalimbali wakati wa matukio yajayo.

Wakati wa mkutano huo, alihakikisha kuonesha historia ya kazi ya kampuni huko Misri, ambayo inafanya kazi mara kwa mara tangu Mwaka 1958 na anaheshimiwa kuwa mwakilishi wake huko Misri kwa mwaka 1989, akiashiria kuwa kampuni hiyo haikushuhudia kukomeshwa wakati huo isipokuwa kipindi cha mapinduzi na kwamba alifanikiwa kuirudisha kazini tena.

Mwishoni mwa mkutano, “Gendi” alisisitiza kuwa “milango yetu iko wazi kwa mapendekezo yote, kuchunguza uwezekano wa matumizi yao, akibainisha kuwa tuliwezesha njia zote za mawasiliano na Wamisri nje ya nchi, kwa njia zote zinazowezekana, kwa uzoefu wao na taaluma zao tofauti, na kwamba sisi tuna furaha kwa uendelevu wa shughuli za kampuni ya kiromania katika Misri na upanuzi wake, kutumikia wana wa Misri katika Romania kama vile jumuiya za kiarabu waliopo kwenye ardhi yake zinazotumia ndege za Kiromania na Misri kama kiungo cha mawasiliano na njia ya usafiri kufikia nchi mbalimbali za kiarabu.

زر الذهاب إلى الأعلى