Utambulisho Wa KimisriWahusika Wamisri

Dokta Abdel Malek Odeh

0:00

Ndani ya kurasa za historia kuna wahusika wakubwa wasiowezekana kusahauliwa , basi yeye ni (mwalimu) wa bara la Afrika neno lenye maana ya Mwalimwa kwa lugha ya Kiswahili , kwa mujibu wa mchango wake bora katika masuala ya mifumo ya kisiasa za kiafrika na mahusiano ya kiarabu na kiafrika na nchi za bonde la Nile .

Basi kupitia maandishi yake aliunda shule bora  ya kimisri katika masomo ya kiafrika kwa kipindi kilichozidi kwa miaka Hamsini , na ameweka mtaala kwa shule hii akisema : tunaishi kaskazini mashariki mwa Afrika na tunazungumzia mengi Afrika, lakini hatulielewi isipokuwa kwa kuchanganya  kati ya masomo na uwanja katika mfumo wa taaluma ya kitaasisi ,na tukifikia hilo sasa tunalielewa Afrika kwa haki ya kuelewa ” Vizuri” na kujiweka ndani ya moyo na jicho.

 Kwa Upande wa Utu wake , marehumu akitafuotishwa kwa maadili yake bora na tabasamu lake lisiloacha uso wake, basi kwamba   wanafunzi wake walimwita kwa( mwalimu  mwenye tabasamu ya uso na Mkuu mkubwa) wakati ambapo alitawala vyuo vitatu navyo ni  Uchumi na sayansi za kisiasa vyombo vya habari na tasisi ya mafunzo ya kiafrika, alisifwa kwa sifa ya unyenyekevu mkubwa, uwezo wake wa kiutawala na umakini kwa maana ya kibinadamu kama mfano wa nadra usiokariri.

 Dokta Abd Elmalek  Ali Ahmed Odeh alizaliwa katika mkoa wa Dakahilia  mwezi wa Machi mwaka wa 1927, na alipata shahada ya Sayansi ya kisiasa toka kitivo cha Biashara, Chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1948, na  Shahada ya Uzamili wa Sayansi za kisiasatoka  Chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1951.

Dokta Abd El malek Odeh ameandaa ujumbe wa Uzamivu  wa( uzito wa kiisilamu), lakini daktari Abd El kader Hatem amemwomba  ujumbe  mwengine  ili kuendana  mwelekeo mkuu  kwa nchi  katika umakini kwa masuala ya kiafrika , na hatua hii ilikuwa kama mwelekeo wa kugeuka ili awe mtaalamu wa kwanza katika masuala ya kiafrika  kwa kupata Uzamivu wa Falsafa katika Sayansi za kisiasa kutoka chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1956.

  katika muktadha huu daktari Boutrous Ghali “katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa” anasema kwamba nilikutana na daktari Odaa nilipokuwa nikihudhuria majadiliano  yake ya kupata Uzamivu , na alinivutia kwa majadiliano na majibu kwa maprofesa wake, kwa hivyo wakati wa tunapohitaji kuteua mwalimu mpya katika sehemu ya Sayansi ya kisiasa katika kitivo cha Biashara katika chuo kikuu cha Kairo niliwaza jina la daktari Odaa na nikapendelaza achaguliwe kwa baraza la sehamu kwa ujuzi wake  wa kisayansi na ameteuliwa kama mwalimu wa sayansi ya kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1957.

   Dokta alipewa jukumu toka Misri ili kusafiri nchi kadhaa za kiafrika hasa  baada ya uhuru wa Guine Konkere mwaka wa 1958 ili kuangalia  uzoefu wa kujenga chama cha kidemokrasia cha Guine, pamoja na maarifa wake kwa  harakati za ukombozi wa kitaifa ya kiafrika kupitia chama chake  cha jumuyia ya kiafrika iliyomsaidia kujenga njia za mawasiliano na vyombo vya habari ya maarifa ya kiafrika inayopambana ukoloni pia iliyoamini umuhimu wa kurudisha historia kwa Afrika kutoka mtazamo wa kistaarabu wa kiafrika.

Marehemu alielekea katika maisha ya kisayansi  na alikuwa profesa msaidizi wa sayansi za kisiasa mwaka wa 1962,  profesa wa sayansi za kisiasa kutoka mwaka wa 1968 hadi mwaka wa 1978, alifundisha pia huko Marekani kama profesa  Mgeni kwenye  chuo kikuu cha jimbo la Indiana katika kipindi cha 1965-1964, na alifanya kazi kama profesa katika taasisi ya utafiti  na mafunzo ya kiafrika chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1974, kisha alitawala Ukuu wa kitivo cha habari chuo kikuu cha Kairo 1971-1979 na rais wa sehemu ya sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo .

 Alisafiri Marekani ili  kufanya kazi kama profesa mgeni katika chuo kikuu cha New York   (stoni brok) Marekani mwaka wa 1979-1978, na aliporudi kutoka Marekani alitawala ukuu wa kitivo cha habari chuo kikuu cha Kairo 1981-1979, na wakati huo huo Mkuu wa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo 1981-1980 na mkuu wa taasisi ya utafiti na mafunzo ya kiafrika chuo kikuu cha Kairo 1981 .

  Alifundisha pia nje ya jumhuri ya kimisri kama profesa wa sayansi ya kisiasa na mashauri wa chuo kikuu cha sanaa kwa masuala ya kitataaluma(jumhuri ya yaman) katika kipindi cha 1985-1981, aliporudi alikuwa profesa wa wakati wote “bure” katika kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa chuo kikuu cha Kairo mwaka wa 1978.

Alishikia nafasi kadhaa za kisayansi akiwa ni pamoja na Mwandishi  mkuu wa habari ya gazeti la kimataifa lililochapishwa toka Taasisi ya  El Ahram  1980-1956 ,  ambapo alishirikiana na Dokta Buotros Ghali katika kuanzisha gazeti la kwanza lilichapishwa mwezi wa Julai 1965.

 Dokta Ali Eldin Helal “profesa ya sayansi ya kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo” alieleza kwamba Dokta Odaa alishiriki katika kuweka misingi ya kazi katika Gazeti la siasa ya kimataifa , kuandaa maudhui zake na kuchagua vijana watafiti na kwenye kurasa zake huchapishwa  makumi ya  tafiti na ripoti kwa hiyo, siyo ziada kwa  kusema  kwamba  siasa za kimataifa zinarejeshwa kwake  na Dokta  Buotros Ghali  kwa mwendelezo wake.

Mnamo mwaka wa 1970 alikuwa mshauri wa waziri wa zamani sana wa  vyombo vya habari Bwana( Mohamed Hassanien Heikal) kisha mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya kisiasa na mikakati katika al-Ahram Kairo 1975-1974, na alitawala  msaidizi wa mwandishi mkuu wa habari  na rais wa idara ya taasisi Al ahram Kairo 1974-1971 .

Pamoja na kufanya kazi katika nafasi kadhaa za kimataifa mnamo kipindi cha 1978-1976 alitawala nafasi ya Sekertari mtendaji wa mfuko wa sanduku la kiarabu kwa msaada wa kiufundi  kwa Afrika- katiba kuu ya mkusanyiko  wa nchi za kiarabu ,alikuwa mshauri wa masuala ya taasisi ya kimataifa na kitaifa- wizara wa mambo ya ndani nchini  Bahrin 1991-1967 , pia alishiriki katika kamati maalumu ya utafiti wa mgogoro barani Afrika, chuo kikuu cha umoja wa mataifa huko Tokyo 1985-1984 ,na  pia alitawala  nafasi ya makamu wa rais wa  chama cha  kiafrika kwa sayansi za kisiasa.

 Alikuwa msaidizi kwa  kamati ya sayansi ya kisiasa kwa  baraza kuu la utamaduni huko Kairo 1991-1992, alikuwa pia mwanachama wa mjadala wa utafiti migogoro barani Afrika  ulioandaliwa kwa  Umoja wa mataifa na chuo kikuu cha Umoja wa mataifa  huko Tokyo, na alikuwa  mwanachama wa mkutano wa kiafrika ulioandaliwa kwa  tasisi ya UNISCO huko Paris ili kutafiti masuala ya Afrika kwa mustakbali mnamo mwaka wa  1955, na alijiunga na baraza la kimisri kwa mambo  ya nje 1999 .

Dokta Odaa amekuwa mwanachama wa vyama kadhaa kwa ndani na kimataifa na ikijumulisha uanachama wa Jumuia  ya kimataifa kwa  mafunzo ya vyombo vya habari na mawasiliano (Marekani) , mwanachama wa taasisi ya kiafrika (Misri ) , taasisi ya kimisri kwa sayansi ya kisiasa , taasisi ya kimsri wa uchumi na Sheria, taasisi ya kimsri kwa kanuni ya kimataifa na taasisi ya kiarabu kwa Sayansi za kisiasa .

Profesa Abd Elmalek Odda alisifu kwa sifa nyingi nzuri basi kwamba  yeye ni mwalimu mwenye uso wa tabasamu ambapo alikuwa ametendana  na wanafunzi wake kwa mtindo unaojumuisha Uongozi  na huruma ya baba na wanafunzi wake wanakumbuka msimamo wake katika kuwasaidia wanaojihusisha katika shughuli za kisiasa katika vyuo vikuu katika kukabili huduma za usalama na ushindi wake kwa haki za wanafunzi za harakati  za  uhuru wao wa kueleza maoni yao na misimamo yao ya kisiasa  na katika mfumo huu mwandishi wa habari “Saeed Elshahat” aliyekuwa Mwanaharakati katika Klabu ya Mawazo ya Nasserist katika chuo kikuu mwaka 1981 anaeleza kwamba wakati marehemu alikuwa profesa wa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa , alimwokoa kutoka mkono wa Meja wa Usalama wa Nchi aliyemkamata na wanafunzi wengine kwa sababu wao walikuwa wamesambaza vipeperushi vinawasisimua wanafunzi kwa kukataa uchaguzi wa Umoja wa wanafunzi  katika Maandamano dhidi ya kuwepo wa Ulinzi  wa chuo kikuu.

Dokta Abd Elmalek Odda amejitetea haki za wanafunzi za kujieleza maoni yao na alikataa uingiliaji wa Ulinzi  wa chuo kikuu katika masuala ya wanafunzi na ameruhusu haki ya kuandamana na kusambaza vipeperushi , hayo yote yalitokea mnamo miaka ya Themanini wakati  ambapo yote hayakuruhusiwa na alikuwa amesikiliza kwa shauku kubwa kwa wanafunzi wake wakati wao walikuwa wamempinga na wamemjadili na yeye alikuwa amejibu na tabasamu pana  kwa upendo na furaha ambapo ni baba , mwalimu na mtaalamu.

Na sifa ya unyenyekevu inazingatia moja ya  sifa muhimu zinazotofautisha mhusika  wake ambapo ni mojawapo wachache ambao hakuna anayepingana na Thamani yao ya kisayansi na tabia zao nzuri  za kibinadamu na angalau mnamo  kipindi Fulani  yeye alikuwa Mkuu  wa  vitivo vitatu navyo  ni kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa , kitivo cha habari na taasisi ya mafunzo ya kiafrika katika wakati mmoja lakini sifa ya unyenyekevu ilikuwa mojawapo sifa muhimu zinazotofautisha mhusika wake .

Profesa Hamdy Abd Elrahman “profesa wa sayansi za kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo”  anasema kwamba Ni nadra na isiyo ya kawaida kwamba tunapata anayekuwa na unyenyekevu kama huu na wanafunzi na wenzake na yeye hamruhusu mtu yeyote kubeba mkoba wake lakini yeye anaubeba mwenyewe na ninakumbuka kwamba mimi nilikuwa naye mjini Khartoum mwanzoni mwa miaka ya tisini ili kuhudhuria mkutano wa kisayansi kuhusu Ukamilifu barani  Afrika ambapo alikuwa hakuketi mbele ya bodi hata mimi nilihisi haya kwa kukaa kwake  katika safu za mwisho na nimeshangaa  kutoka unyenyekevu wake mkubwa.

Na hivyo ndivyo profesa Mahmoud Abo Elenin “profesa wa sayansi za kisiasa na mkuu wa zamani wa taasisi ya mafunzo na utafiti ya kiafrika” amesisitiza kwa msemo wake : sisahau wakati nilikwenda kwa

Maktaba ya kitivo cha Uchumi na nimengoja dakika kadhaa katika ofisi ya Sekretari kwa shughuli  zake na wageni wake ofisini na wakati alikuwa ametoka ili kuwaaga ، Jicho lake likanijia na akasema :tangu lini na wewe yupo hapa ? Mimi nimejibu : tangu dakika kadhaa

Na alisema : sina maprofesa wanaketi nje !! lakini yeye amemfunza kitu muhimu nimekifanya wakati nilikuwa Mkuu wa taasisi

Hayo ni pamoja na uwezo wake wa mawasiliano ya kijamii na pande zote  iliyomfanya kuwa mwenye thamani na wa kimo cha kisayansi na kibinadamu ambayo ni nadra kukaririwa , ambapo aliweka  mgusa na alama zake wazi katika nyanja ya sayansi za kisiasa kwa ujumla na nyanja ya mafunzo ya kiafrika hasa na wakati wote alishughulikia kwa masuala na matatizo ya nchi na wanafunzi wake wameeneza katika taasisi mbalimbali za dola na mashirika , vyuo vikuu , vituo vya utafiti , wizara ya mambo ya nje , vyombo vya habari vinavyosemwa , vinavyosikiwa na vinavyoonwa ,  katika Mkusanyiko wa Nchi za Kiarabu na katika ndani na nje ya misri ambapo alikuwa na wanafunzi kutoka ndugu waarabu na waafrika na Licha ya tofauti hii , aliweza kuwasiliana na wote na Kuuliza juu yao na kuwashiriki furaha na huzuni zao.

Na katika muktadha huu , Dokta Mostafa Elfeky anasema wakati niliomba kusoma  katika chuo kikuu cha London katika mwaka wa 1971, profesa Abd Elmalek Odda alikuwa amemtuma  Kwangu  kumpendekeza kwake na kwa profesa wangu Botros Botros Ghali Kujaza hati zinazohitajika ili kuandikisha katika kitivo cha mafunzo ya mashariki na kiafrika na marehemu Alikuwa Mwanazilishi wa Familia ya Nile na ambaye alitupa kutoka ujuzi wake  kile wengine wanakiuma na wanafunzi wake wanamkaribia kwa njia sio kawaida ambapo Maelfu yalifurika baba yake  na alisambaza ufahamu wa masomo ya kiafrika na kimataifa katika wakati mmoja, na mimi bado nakumbuka ziara yake kwangu katika london na mimi ni mwanadiplomasia  katika ubalozi wa kimisri katika asubuhi na mwanafunzi katika chuo kikuu cha London jioni na jinsi ushauri wake ghali ulivyokuwa kama kitu adhimu sana katika Hali ngumu  zile.

Na marehemu alikuwa amejipambanua kwa Ukali wa kiteknolojia na kitaaluma na  aliwakabidhi kwa kila mtu aliyefanya kazi naye , kwa hiyo Mfano wa uchambuzi uliotolewa na Dokta Odda kwa wanafunzi wake ili kufunza ukweli wa kisiasa unajumuisha vipengele vitatu ambavyo ni historia , ufahamu wake na Mtaala na kufuata sheria zake ,vyombo ambavyo mtafiti anavitumia ili kufikia ukweli na kuchambua zaidi ya habari na maelezo ambapo alikabiliana na masuala ya sehemu katika kiwango kidogo na kwa kiwango sawa cha ufanisi katika kushughulikia masuala ya kisiasa katika kiwango cha ujumla ambavyo kinatoa  uaminifu zaidi kwa uchambuzi wa kisiasa

Kama marehemu anajulikana katika uwezo wake wa kisayansi na utafiti alikuwa wa kidato cha kwanza, na alithibitisha mafanikio yaliyopatikana katika nafasi mbali mbali alizozishikilia, alikuwa mkuu wa maprofesa , ambapo alikuwa mkuu wa Kitivo cha Uchumi na Sayansi za kisiasa , Kitivo cha Habari na Taasisi ya Mafunzo ya Afrika, na licha ya uwezo wake bora wa kiutawala Katika siku ya kukandamiza ukandamizaji wa wasaidizi au uwekaji wa vikwazo au vikwazo dhidi yao, alikuwa na mwelekeo zaidi wa utawala wa kibinadamu, ambao ulionekana kama bora kufikia malengo ambayo ukatili na nguvu haziwezi kufikia.

 Kwa hivyo, ukubwa wa mwanadamu ulikuwa moja ya vifunguo muhimu kwa mhusika wake na labda alizingatia mawasiliano ya kibinadamu na mahusiano mema ya kibinadamu kama lango la kuhakikisha kwa mafanikio yoyote ya kisayansi.

Dokta  Odda alipewa Nishani ya Daraja la Kwanza la Sayansi na Sanaa mnamo 1987 kwa kutambua michango yake ya kielimu katika uwanja wa mafunzo ya Kiafrika.  Pia sherehe moja ilifanyika katika baraza kuu la Utamaduni katika Kairo mwaka wa 2009 wakati wa kuzaliwa kwake kwa miaka ya Themanini ambapo wataalamu wengu wa Sayansi za kisiasa waliihudhuria , wakati ambapo Dokta Mustafa El fiky alisema:  “Tunakusalimu, baba wa watoto hao watatu, Dokta wawili Jihad na Hisham, na wa tatu ni kila mmoja wetu katika wanafunzi wako katika miongo mitano iliyopita! Ulibarikiwa na mfano wa kutoa, mfano wa udhamini na ishara ya  ubaba, Mwenyezi  Mungu aliongeza maisha yako na kukupa vile vile ulivyotoa nchi na vizazi mfululizo.”

Sherehe ya kumheshimu katika Chuo Kikuu cha Kairo katika ukumbi mkuu wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti na Mafunzo ya kiafrika iliyofanyika mnamo Machi 27, 2013, katika hatua ya Profesa Ibrahim Nasr El-deen, profesa wa sayansi za kisiasa katika chuo kikuu, kuadhimisha mtaalamu yeyote maishani mwake, na alihudhuriwa na kikundi cha wanasayansi, mabalozi, wataalamu, wanadiplomasia na wanaompenda Dokta Abdel Malik Odda kwa kumzingatiwa mkuu wa  masomo ya Kiafrika tangu miaka ya hamsini, akihudhuriwa na kikundi cha maprofesa wa sayansi ya kisiasa nchini Misri na ulimwengu wa Kiarabu,  kama Dokta Ali al-Din Hilal, Dokta Saif Al-Din Abdel-Fattah, Dokta Mustafa Alawi, Dokta Kamal Al-Menoufi, Dokta Helmy Shaarawy, Dokta Ahmed Youssef Al-Qurai, Dokta Ikram Badr Al-Din, Dokta Mahmoud Abu El-Enein, Dokta Farag Abdel-Fattah  , Mabalozi wa Kiafrika, wataalamu,wanadiplomasia na vyombo vya habari, na umati mkubwa wa wanafunzi wa mafunzo ya Kiafrika na bara la Afrika, na wengine wengi, ilikuwa sherehe ya kihistoria kwa maana kamili ya neno hilo katika maisha ya wataalamu  wa sayansi za kisiasa.

Kitivo cha Uchumi na sayansi za kisiasa katika chuo kikuu cha Kairo kilipanga Huduma ya ukumbusho ya Dokta Abd Elmalek Odda profesa wa zamani wa kitivo katika tarehe ya tano mwezi wa kwanza mwaka 2014 na hivyo kwa kuhudhuria Dokta Hala Elsaeed profesa wa kitivo ,  Dokta Gaber Nassar mkuu wa chuo kikuu cha Kairo na marehemu Dokta Botros Botros Ghali Rais wa heshima wa Jumuiya ya Haki za Binadamu pamoja na idadi kadhaa za washiriki wa Kitivo

Na inafahamika kwamba Dokta Hala Elsaeed profesa wa kitivo cha Uchumi na sayansi za kisiasa na zamani katika chuo kikuu cha Kairo Alizindua jina la marehemu kwenye ukumbi wa namba ya 5 kitivoni Kwa kumtambua na kumkumbuka hasa Dokta Odda alitoa maktaba yake ya zamani inayojumuisha takriban vitabu elfu kumi na tano kwa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa na kutoka upande wake Dokta Gehad Odda ambaye alitoa neno la familia ya Dokta marehemu  Abd Elmalek Odda aliushukuru usimamizi wa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa kwa sherehe ya kuheshimiwa ya baba yake na kumkumbuka

Chama cha wahitimu wa  vyombo vya habari katika kitivo Cha habari katika chuo kikuu cha Kairo kilipanga sherehe ya ukumbusho ya Dokta Abd Elmalek Odda profesa wa kitivo cha habari wa zamani , hii hasa wahitimu wa kitivo wanamkumbuka marehemu kwa kumbukumbu zisizosahauliwa kuhusu mahusiano yake mema yaliyokuwa kati ya  wanafunzi na profesa wao wa chuo kikuu na Dokta Hassan Emad Mekawy na Idadi kadhaa za maprofesa ya kitivo na miongoni mwao : Dokta Magy Elhalawany , Laila Abd Elmegeed ,  Ali Agwaa ,  familia ya marehemu  na maprofesa wa kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa na taasisi ya mafunzo na utafiti ya kiafrika wameihudhuria

Na hitimisho , Hakuna neno katika lugha linaloweza kumsifu marehemu profesa Abdel Odda ambapo Alikuwa mfano bora wa Kile kinachopaswa kuwa na  profesa kutoka sifa nzuri na kile kinachopaswa kuwa profesa wa   uzani na lazima anajishughulikia na masuala yote ya nchi katika daraja la kwanza na kile kinachopaswa kuwa  raia mmisri wa asili alihusishwa na mizizi yake, basi kumbukumbu kwake kutabaki hai kwa historia yote na kile ametoa kutoka urithi wa kisayansi na michango ambayo haijawahi kutekelezwa hasa katika uwanja wa masomo ya kiafrika.

Back to top button