Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pembezoni mwa kazi za Baraza la kiutendaji la Umoja wa Afrika
Ali Mahmoud
Bw. Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, alikutana Alhamisi, Februari 16, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Christophe Lutendula, pembezoni mwa kikao cha 42 cha Baraza la kiutendaji la Umoja wa Afrika.
Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa mawaziri hao wawili, wakati wa mkutano huo, walisisitizia umuhimu wa kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika ngazi mbalimbali, ambapo walikaribisha ukuaji wa kiwango cha mahusiano ya nchi mbili mnamo miaka ya hivi karibuni, akibainisha umuhimu wa kufanya kazi ili kuboresha uhusiano huo kwa upeo mpana kufikia maslahi ya watu wawili ndugu.
Pande hizo mbili pia walionesha nia ya kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kulingana na tamaa ya nchi hizo mbili, sio tu kuongeza kubadilishana biashara, lakini pia ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji, wakiashiria umuhimu wa kutekeleza Mkataba wa Biashara Huria ya Afrika, itakayoongeza kiwango cha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ameongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje amesisitiza Mshikamano wa Misri na serikali ya Congo katika kukabiliana na makundi ya kigaidi, akisifu juhudi zinazofanywa na Rais wa Congo “Tshisekedi” katika kuunga mkono juhudi za maendeleo na kukuza utulivu nchini Congo.
Hivyo, Waziri Sameh Shoukry aliashiria utayari wa upande wa Misri kushirikiana katika uwanja wa kuhamisha utaalamu wa Misri katika sekta zenye maslahi kwa upande wa Congo, na nia yake ya kuchunguza uwezekano unaopatikana kwa ajili ya ushiriki wa makampuni zaidi ya Misri yanayofanya kazi katika nyanja za ujenzi katika miradi iliyopo nchini Congo ya Kidemokrasia.