Waziri wa Umwagiliaji akagua hifadhi ya zamani ya Aswan na Kituo cha Utamaduni cha Afrika huko Aswan
Mervet Sakr
Ndani ya mfumo wa ziara yake katika Mkoa wa Aswan… Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, Prof. Hany Swailem, alikagua hifadhi ya zamani ya Aswan na Kituo cha Utamaduni cha Afrika kilichopo Aswan.
Dkt. Swailem alisema kuwa yuko makini kufuatilia hali ya ujenzi wa vituo vyote vya maji nchi nzima ili kuhakikisha hali zao hususan Bwawa la Juu na hifadhi ya zamani ya Aswan.
Dkt. Swailem pia alikagua Kituo cha Utamaduni cha Afrika huko Aswan, ambacho ni moja ya maeneo maarufu ya utalii huko Aswan, ambapo kituo hicho kinajumuisha michoro mingi, mikusanyiko na filamu za maandishi zinazowakilisha ustaarabu na utamaduni wa nchi za Kiafrika na mila na desturi za watu wa Afrika, na maktaba ya maandishi inayojumuisha vitabu vingi na albamu za akiolojia na kihistoria zinazoelezea historia ya Mto Nile, pamoja na ukumbi wa wazi wa Kirumi.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji imeanzisha Kituo cha Utamaduni cha Afrika huko Aswan, na hapo awali kilijulikana kama Makumbusho ya Mto Nile kuendelezwa na kugeuzwa kuwa Kituo cha Utamaduni cha Afrika, na kuongezwa kwa miliki nyingi zinazowakilisha ustaarabu na utamaduni wa nchi za Kiafrika na mila na desturi za watu wa Afrika kuwa nyongeza muhimu ya kitamaduni huko Aswan inayoonesha tamaduni za nchi mbalimbali za Kiafrika, na kituo hicho kinajumuisha nafasi tano tofauti, ambazo kila moja ina michoro, umiliki na filamu za maandishi kwa nchi za Afrika, na ina maktaba ya maandishi ambayo inajumuisha Vitabu vingi vya akiolojia na kihistoria na albamu zinazoelezea historia ya Mto Nile, na utekelezaji wa ukumbi wa wazi wa Kirumi umekamilika kama moja ya vipengele vya kituo hicho.