Habari
Al-Azhar yatoa wito wa kuuwepo kwa kampeni ya kimataifa ya kutoa misaada kwa watu wa Sudan
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Al-Azhar, Prof.Ahmed Al-Tayeb, alitoa wito kwa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kuharakisha misaada ya watu ndugu wa Sudan; kuwaokoa kutokana na janga la vita, migogoro, njaa na kuenea kwa magonjwa na majanga, na kupitisha kampeni ya misaada ya kimataifa ili kutoa aina zote za msaada kwa watu wa Sudan katika hali hizi ngumu na zenye uchungu.