Habari Tofauti

83% HALMASHAURI WATENGA FEDHA KWA AJILI YA AFUA ZA LISHE NCHINI

Angela Msimbira

0:00

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali  za Mitaa

Adolf Ndunguru amesema  Serikali  imeendelea kusimamia na kuhakikisha fedha  zinatengwa na kutolewa  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo kwa wastani wa kitaifa kwa mwaka wa fedha 2022/23 tumefikia asilimia 86.69 ya utekelezaji wa bajeti ya lishe ukilinganisha na asilimia 22 ya mwaka wa fedha 2017/18 wakati kunasaini Mkataba wa lishe nchini.

Ameeleza hayo wakati akitoa  mrejesho wa utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni, 2023, uliosainiwa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa niaba ya Mheshimiwa Rais tangu Desemba, 2017  kwenye  mkutano wa Tathmini  ya saba  ya utekelezaji wa mkataba wa lishe  unaofanyika katika ukumbi wa Jiji la Dodoma, Mtumba jijini Dodoma

Amezitaja Halmashauri tano ambazo  haikuweza kuchangia  fedha hizo kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mkalama, Uyui  na Lushoto nakuziagiza  kuhakikisha  kufanyia mapitio ya bajenti ya mwezi Disemba  na kuingiza fedha inayotakiwa  kukidhi matakwa ya Serikali ya kutenga kiasi cha shilingi 1000 kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

Aidha,  amesema kumekuwa na ongezeko la bajeti ya shughuli za Lishe katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutoka shilingi bilioni 13.5 kwa mwaka wa fedha 2022/23 hadi bilioni 14.8 kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Back to top button