Habari

ISAIDIENI SERIKALI UKUSANYAJI WA MAPATO

OFISA Elimu Mkoa wa  Shinyanga Dafroza Ndalichako amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kuisaidia Serikali katika ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo katika maeneo yao.

Akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao leo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Ndalichako amesema pamoja na majukumu walionayo ya shughulikia na kutatua kero za wananchi wana wajibu wa kuisaidia Serikali katika ukusanyaji wa mapato, kuvijua vyanzo vipya vya mapato na kuwa wabunifu   katika maeneo yao ili kuisaidia Serikali katika kupanga maendeleo na kupeleka huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake,   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI  Hamis Mkunga amesema Mikoa 12 imeshapatiwa mafunzo hayo  na lengo la Serikali ni kufika katika Mikoa yote ili kuboresha utendaji kazi wa viongozi hao.

Naye, Mtendaji wa Kata Mwamashele, Tarafa ya Negezi, Halmashauri ya Wilaya ya  Kishapu, Lilian Chungaraza amesema mafunzo hayo waliopatiwa yamekuwa ni nyongeza ya yale waliokuwa nayo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma.

زر الذهاب إلى الأعلى