Habari Tofauti

Halmashauri ya Mji Njombe imeendelea kupiga hatua kufikia malengo ya kutokomeza udumavu Mkoani Njombe.

Akiwasilisha taarifa ya Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe katika Halmashauri ya Mji Njombe Julai 17 ,2023 Afisa lishe Fransisca Mosha amesema,katika kipindi cha miezi mitatu (April – June, 2023) wamefanikiwa kutengeneza mbadala wa chakula tiba (locally made therapeutic milk) kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye utapiamlo. Chakula tiba hicho kimefanya vizuri na kitaenda kupunguza utegemezi kutoka bohari kuu ya dawa(MSD).

Afisa Lishe Fransisca amesema katika kupambana na changamoto ya udumavu kwa watoto mkoani njombe Halmashauri ya Mji Njombe wameendelea kutoa elimu ya matibabu ya utapiamlo na katika kipindi cha miezi mitatu(3)wamewez kutoa elimu hiyo ya matibabu ya utapiamlo kwenye vituo sita(6) vilivyopo Halmashauri ya mji Njombe na jumla ya watoto watano (5) waliokuwa na tatizo la utapiamlo mkali kutoka maeneo mbalimbali wametibiwa na kupona.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt Yesaya Mwasubila ametoa rai kwa akina mama wajawazito kuzingatia mahudhurio ya kliniki wakati wote wa ujauzito hasa kufanya hudhurio la kwanza mapema,pamoja na kutumia dawa za kuongeza damu zinazotolewa ili kuimarisha afya za watoto kabla yakuzaliwa.

Dkt Yesaya Mwasubila pia ametoa msisitizo kwa wataalamu wanaofanya kazi kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya ,kuhakikisha wanawapatia mama wajawazito elimu ya lishe pamoja na dawa zote wanazohitajika kupatiwa kwa kila hudhurio la kliniki linalofanyika.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Gwakisa ,Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Ndg.Agatha Mhaiki amesisitiza ushirikiano wa kutoa taarifa sahihi kwa ngazi zote kuanzia vijiji, kata mashuleni hadi mkoa ili kuwezesha kampeni ya kutokomeza udumavu mkoani njombe kufanikiwa.

Kwa suala la kushiriki na kufanya mikutano ya kuhamasisha kuhusu Lishe Bora ngazi ya kata Katibu Tawala wilaya ya njombe Agatha Mhaiki amewataka watenda

زر الذهاب إلى الأعلى