Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA ZANZIBAR IKO TAYARI KUPOKEA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imejiandaa  kuhakikisha Zanzibar inakuwa mstari wa mbele  kuyapokea mabadiliko ya teknolojia  ambayo ni msingi muhimu kwa kukuza na kuendeleza uchumi wa kisasa pamoja na kurahisisha maisha ya wananchi wa hali zote.

Ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa kidijitali wa Serikali na Mfumo wa Bajeti na Matumizi Serikalini (BAMAS)  uliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema matumizi ya mifumo ya TEHAMA yataleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika utendaji kazi wa Serikali kwa ulazima wa kutumia mifumo hiyo  kwa  kuwa matumizi ya TEHAMA yataimarisha ukusanyaji wa mapato, kurahishisha utoaji wa huduma  sekta ya Afya, Elimu , kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kukomesha vitendo vya wizi, kuzuia rushwa na ubadhirifu pamoja na kuimairisha usalama wa nchi.

Vile vile amesema mfumo wa BAMAS umeleta uwazi kwenye matumizi Serikalini, utaimarisha uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali, umewezesha mifumo yote ya malipo na matumizi ya fedha za Serikali  kusomana kwa haraka na  kwa ufanisi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

زر الذهاب إلى الأعلى